Msanii ‘Banza Stone’, Ramadhan Masanja Azikwa Dar

Msanii Ramadhani Masanja au maarufu kwa jina la Banza Stone

Msanii Ramadhani Masanja au maarufu kwa jina la Banza Stone

 Jeneza lenye mwili wa marehemu  Ramadhani Masanja "Banza Stone" likitolewa nyumbani tayari kwa mazishi Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Ramadhani Masanja “Banza Stone” likitolewa nyumbani tayari kwa mazishi Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

MSANII nyota wa muziki wa dansi nchini aliyefariki dunia jana jijini Dar es Salaam, Ramadhani Masanja au maarufu kwa jina la Banza Stone amezikwa leo jioni katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salamm. Mazishi ya Banza Stone ambayo yamehudhuriwa na baadhi ya wasanii nyota, viongozi ambalimbali na wananchi yamevuta hisia za wengi hasa wapenzi wa muziki wa dansi. Tayari baadhi ya wasanii nyota na nguli wa dansi akiwemo Kalala Jr, Jose Mara, Halid Chokoraa, Muumini Mwinjuma na wengine wametunga wimbo maalumu wa kumsindikiza nguli huyo wa utunzi na uimbaji nchini.

Hata hivyo msanii huyo ataendelea kukumbukwa kwa tungo na nyimbo zake zilizovuma kama zile za ‘Mtaji wa Masikini’, Ujafa Ujasifiwa, ‘Unapotaka Kuanza Maisha’, na Mtu Pesa’ na nyinginezo. Pamoja na hivyo msanii huyo atabaki katika kumbukumbu pia kutokana na kauli tata ambazo aliwahi kuzitoa enzi za uhai wake.

Miongoni mwa kauli hizo ni pamoja na ile ya kwamba; ‘ameota akiwa usingizini kwamba amekaribia kufa, na kwamba kifo chake kitatokana na kuungua gafla kisha kufariki dunia’. Kauli nyingine ni pale aliposema kuwa yeye ni marehemu mtarajiwa na kinachomfanya aendelee kupumua ni kwa sababu ana roho ya paka, kauli aliyoitoa baada ya kuzushiwa kifo na baadhi ya watu akiwa yungali hai. Kauli nyingine ni ile ya kufunga ndoa kimyakimya bila ya watu hasa wasanii wenzake kujua.