Msafara wa Sekretarieti ya Taifa ya CCM Wawasili Kigoma

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na msafara wake, wakikaribishwa na viongozi wa CCM mkoa wa Kigoma baada ya treni kutoka Dar es Salaam, kuwasili leo asubuhi mjini Kigoma, Wanaoshuka ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma. (Picha na Bashir Nkoromo).

Abiria kutoka Tabora kwenda Kigoma wakiwa katika behewa leo

Makatibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia) na wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kulia) wakinunua chakula kwa mamalishe, kwenye stendi ya Saranda mkoani Singida, daaba ya kuwasili kwenye stesheni hiyo, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. (Picha na Bashir Nkoromo)

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mstaafu John Chiligati wakishiriki kucheza ngoma ya wakazi wa mkoa wa Singida, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Martine Shigela.(Picha na Bashir Nkoromo).