
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Siasa Ndugu Nape Mosses Nnauye ukiwasili katika mji wa Nzega Katika wilaya hiyo Tayari kwa kuanza Ziara ya Siku 18 katikia mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara kesho ambapo ziara hiyo itaanza katika mkoa wa Shinyanga, Katibu Mkuu huyo amepokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na wananchi waliojitokeza katika mapokezi hayo, Kinana amezungumza na wananchi wa Nzega na kukutana na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali ambapo pia amepokea Pikipiki tisa kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo Dk. Khamis Kigwangala ambazo ambazo amezikabidhi kwa viongozi wa kata 9 kati ya 21 zilizopo katika Wilaya hiyo, ambapo pia amekabidhi mashine ya kutotolea vifaranga vya kuku kwa kikundi cha wazee wa Nzega, Pikipiki hizo zimekabidhiwa katika kata za Budushi, Ndala, Puge, Nkininziwa, Mbogwe, Lusu, Ijaniga, Utwigu na Isanzu baadae pikipiki 7 zitafutaiwa na kisha kata tano za mwisho.
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanachama mbalimbali na wananchi mara baada ya kuwasili wilayani Nzega. Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukisalimiana na wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa ujenzi wa vibanda vya biashara katika uwanja wa Samora, vibanda hivyo ni mradi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Nzega.
Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala akizungumza na wananchi huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Siasa Ndugu Nape Mosses Nnauye huku katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipiga makofi
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi huku Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala akimsikiliza.
Wananchi wa Nzega wakiimba kwa furaha mara baada ya kumpokea katika mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana.
Umati wa wanavikundi wakiwa katika mkutano huo
Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala akimsikiliza akiongea na wananchi.
Pikipiki zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala akimsikiliza zikiwa tayari kwa ajili ya kukabidhiwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki kwa Hanifa Musa Kutoka kata ya Isanzu huku Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala katikati akishuhudia tukio hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Nzega Dk. Khamis Kigwangala mara baada ya kukabidhi mashine ya kutotolea vifaranga kwa kikundi cha wazee wa Nzega mjini humo.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Siasa Ndugu Nape Mosses Nnauye akizunumza na wana Nzega. Katibu Mkuu wa CCM. PICHA NA FULLSHANGWE-NZEGA.