Mrembo Ahukumiwa Kwenda Jela kwa Kumtusi Rais

Merve Buyuksarac, mwenye umri wa miaka 27 alipatikana na hatia ya kumtukana hadharani afisa huyo mkuu wa serikali

Merve Buyuksarac, mwenye umri wa miaka 27 alipatikana na hatia ya kumtukana hadharani afisa huyo mkuu wa serikali

MAHAKAMA moja mjini Istanbul imemhukumu kwenda jela mshindi wa zamani wa tuzo ya urembo nchini Uturuki kwa kosa la kumtusi rais wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan.

Malikia huyo wa ulibwende, Merve Buyuksarac amehukumiwa kifungo cha miezi 14 gerezani. Bi. Buyuksarac, mwenye umri wa miaka 27 alipatikana na hatia ya kumtukana hadharani Mkuu wa nchi hiyo na serikali.

Taarifa zinasema kuwa aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii pamoja na kuwatumia watu shairi lenye matusi katika mtandao wake wa Instagram.

Hata hivyo tayari wakili wa mrembo huyo amepinga hukumu hiyo katika Mahakama Kuu ya Bara la Ulaya kwa kutoridhika nayo. Pia Bi. Buyuksarac, amekanusha madai yote dhidi yake.

Wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu wanasema kuwa kesi hiyo ni mojawapo ya njia ya serikali ya rais Erdogan kukandamiza uhuru wa kujieleza.

Hadi kufikia sasa takriban watu 2,000 wengi wao wasanii nyota na hata wanafunzi wameshtakiwa kwa kumkejeli au hata kumtusi rais huyo tangu mwaka wa 2014.

Hukumu hiyo imehahirishwa ikimtaka mtuhumiwa asirudie makosa hayo katika kipindi cha miaka mitano.