MWENYEKITI wa Taifa wa TLP, Augustino Lyatonga Mrema ameibuka na kumtuhumu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Shariff Hamad anatumia njia zisizo sahihi kutaka kuingia madarakani kutokana na maneno ambayo amekuwa akiyatoa mara kadhaa katika kauli zake.
Mrema ametoa tuhuma hizo leo akizungumza na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam na kudai kuwa kauli anazotoa Seif ni hatari kwa taifa na Zanzibar hivyo inabidi achukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kushtakiwa endapo akiendelea.
Mrema alisema Maalim Seif anatangaza ataingia madarakani kwa nafasi ya urais kabla ya mwaka 2020 jambo ambalo linaashiria ataingia kinyume cha sheria za uchaguzi na wakati alishiriki kuhamasisha wananchi wanachama wa CUF kususia uchaguzi uliopita na kuwafanya wakose ajira huku yeye akiendelea kuneemeka na malipo ya penseni ya Umakamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Aliongeza kuwa jambo hilo linatishia uhai wa chama kwani kinaweza kusambaratika kutokana na kutojihusisha na uchaguzi hivyo kuwaomba wananchi wa Zanzibar kupuuza kauli zinazotolewa na kiongozi huyo zinazoweza kuleta uchochezi.
Aidha TLP ya Mrema imelaani kitendo cha baadhi ya wafadhili kusitisha misaada kwa nchi kutokana na uchaguzi wa Zanzibar na Sheria ya Makosa ya Mtandao kwa madai kitendo cha wafadhili hao ni sawa na kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine. Alisema mgogoro katika uchaguzi katika mataifa yote hata Marekani hutokea lakini sheria na hatua huchukuliwa na taifa husika na si kwa shinikizo la nje.
“…Tunaziomba nchi wahisani kuacha kuingilia masuala ya ndani ya nchi yanayofanyika kwa kuzingatia Katiba za nchi husika. ngozi huyo a