Mrema Aanza Kazi Azungumza na Bodaboda, Ampa Siku Saba Makonda

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema (katikati) akiwa na viongozi wa Chama cha Madereva wa Bajaji na Bodaboda Wilaya ya Kinondoni akisikiliza kero zao leo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanachama na viongozi wa Chama cha Madereva wa Bajaji na Bodaboda Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema alipojitokeza kusikiliza kero zao leo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa viongozi wa Chama cha Madereva wa Bajaji na Bodaboda Wilaya ya Kinondoni akizungumza katika mkutano huo leo Ubungo jijini Dar es Salaam.

MWENYEKITI wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema leo amezungumza na waendesha pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda pamoja na waendesha bajaji wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, na kusikiliza malalamiko mbalimbali dhidi yao.

Akiwakilisha kilio chao, Katibu wa Chama cha Waendesha Bodaboda na Bajaji wa Wilaya ya Kinondoni, George Mbwale alisema licha ya wanasiasa mbalimbali kuwatumia kipindi cha mikutano na kampeni wamekuwa wakiwatelekeza baada ya hapo na hata kushindwa kuwasaidia dhidi ya changamoto anuai za kazi zao.

Alisema wanashangaa kwanini wamezuiwa kufanya kazi zao mjini (kuingia mjini) huku vipo baadhi ya vijiwe na bodaboda zimekuwa zikifanya kazi mjini bila bughudha jambo ambalo linaonesha ama ni miradi ya wakubwa au mazingira ya rushwa kwa wasimamizi wa zoezi hilo.

“…Tumezuiwa kuingia mjini lakini wakati huo huo kuna baadhi yetu wanafanya biashara hiyo katikati ya jiji, sasa tunahoji kwanini sisi tunazuiwa kuna tofauti gani na wao,” alisema Mbwale akizungumzia changamoto za bodaboda.

Baadhi ya wanachama na viongozi wa Chama cha Madereva wa Bajaji na Bodaboda Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema alipojitokeza kusikiliza kero zao leo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanachama na viongozi wa Chama cha Madereva wa Bajaji na Bodaboda Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema alipojitokeza kusikiliza kero zao leo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Alisema wapo tayari kushirikiana na Jeshi la Polisi na wala hawana ugomvi na jeshi hilo lakini kuna vikundi vinavyojiita Shirikishi Vimekuwa vikishirikiana na baadhi ya askari na kunyanyasa waendesha bodaboda. Alisema vimekuwa vikikamata pikipiki kwa mazingira ya hatari tena wakati mwingine zikiwa kwenye mwendo jambo ambalo linahatarisha bodadoda na abiria wake, vikundi hivyo na baadhi ya askari pindi wanapokukamata na kukukuta hauna kosa watakuzungusha hadi utoe chochote jambo ambalo limekuwa kero kwao.

Alisema baadhi ya maeneo askari polisi na vikundi shirikishi vimekosa uadilifu na kufanya kazi hiyo kwa kujiingizia kipato kama vile Tazara Mataa, Buguruni Darajani, Tabata Mataa, Ubungo Mataa, Tiputopu Kituo cha Polisi, Boko Magengeni, Boko Chama, External Mataa, Kawe Darajani na mara nyingine wamekuwa wakiwafuata hadi mitaani.

“…Sisi bodaboda tupo tayari kufuata sheria zote za usafirishaji. Kwanini polisi wanatumia nguvu kubwa kukamata bodaboda kuliko nguvu hiyo kuielekeza katika kutoa elimu ya usalama barabarani, ndio maana hadi leo bodaboda anahisi yeye na polisi ni paka na panya,” alisema Mbwale.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mrema akijibu malalamiko hayo alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ndani ya siku saba ahakikishe bodaboda zilizoweka vijiwe mjini zinaondolewa mara moja ili kuondoa mazingira ya ubaguzi na uonevu kwa zoezi hilo. Aidha amewataka kusaidia kudhibiti rushwa kwa kuorodhesha namba za askari ambao wamekuwa wakiwaomba rushwa na kupeleka ofisini kwake ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mrema ambaye pia na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), amewataka bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani na kusaidiana na vyombo vya usalama kuainisha, makundi maovu ili yaweze kuchukuliwa hatua za kisheria.