Mradi wa tangi la maji wakamilika-Ziwani Pemba

ufunguzi wa kisima

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa
Tangi la Maji la Ziwani Wilaya ya Chake chake Pemba, akiwa katika
ziara ya kutembelea miradi mbali mbali ya kijamii ya Mkoa wa Kusini
Pemba jana.[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]

Tanagi la maji safi kwa ajili ya wakza zaidi ya 17,000

Pichani ni Tangi la Maji safi na Salama lililojengwa katika
shehia ya ziwani wilaya ya Chake chake Pemba,linalouwezo wa kubeba
maji lita 250,000.lenye urefu wa mita 18,ujenzi wa tangi hilo
umefaziliwa Japan ,na UNDP,wananchi mbali mbali wapatao
17,000/-watafaidika na mradi huo.[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]

Rais akiongea baada ya ufunguzi wa tanki yenye ujazo wa lita 250,000

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Wananchi wa Shehia ya
Ziwani na vijiji jirani,wakati wa ufunguzi wa Tangi la Maji la Ziwani
Wilaya ya Chake chake Pemba, akiwa katika ziara ya kutembelea miradi
mbali mbali ya kijamii ya Mkoa wa Kusini Pemba jana.[Picha na Ramadhan
Othman,Pemba.]