Mr Ebbo afariki dunia

MWIMBAJI nguli Tanzania aliyeibuka na staili ya bongofleva kwa ‘tune’ na staili ya Kimasai, Abel Rusheraa Motika, almaarufu – Mr Ebbo amefariki dunia.
Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili alfajiri ya leo zinaeleza kwa Mr. Ebbo alifariki kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa kichomi kwa muda mrefu. Amefariki akiwa nyumbani kwa familia yake, maeneo ya Usa River, Arusha.
Mwanamuziki huyo alifahamika zaidi kwa nyimbo zake zenye lafudhi ya Kimasai, ikiwamo – Mi Mmasai Bwana, Kamongo na nyingine nyingi zilizoteka uwanja wa muziki.
Pia alikuwa miongoni mwa wanamuziki walioinukia kwa kufanya ‘kolabo’ na wanamuziki wengine, hasa wanaotoka Mkoa wa Tanga wakiwamo; Wagozi wa Kaya.
Mipango ya mazishi inafanywa na familia yake na huenda akapumzishwa katika mashamba ya familia yake yaliyoko Usa River.
Gazeti hli tando linatoa pole kwa dunia ya mashabiki wa muziki, marafiki, watoto, ndugu jamaa na marafiki.