Mpishi Maarufu Duniani Kutoka India ‘Ateta’ na Wanahabari

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dk. Aloyce Nzuki (kushoto) akimkaribisha mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India, Sanjeev Kapoor ili azungumze na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam. Mtaalamu huyo alizungumzia umuhimu wa vyakula vya asili katika sekta ya utalii wa utamaduni. Kulia ni Naibu Meneja Mkuu wa Hoteli ya Serena, Daniel Sambai ambayo imegharamia gharama za chakula na maladhi kwa mpishi huyo kwa kipindi chote akiwa nchini. Picha na Anna Nkinda – Maelezo


Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dk. Aloyce Nzuki jijini Dar es Salaam kitabu kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India. Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India.