KAA tayari kwa mpambano wa ngumi wa aina yake ambapo Juni 30, 2013 ikiwa ni wiki ya mwisho kabla ya mwezi wa ramadhan mpambano huo utapigwa. Mabondia wakatili ulingoni na wapole nje ya ulingo kiasi cha kujulikana kama wacha mungu, YOHANA ROBERT na YOHANA MATHAYO watazipiga katika ukumbi wa Friends Corner Hotel, Manzese.
Huu ni mpambano wenye upinzani mkali kutokana na sifa za mabondia wenyewe kutokuwa na mzaha wawapo ulingoni na ni mabondia wasiokubali kushindwa, hiyo nayo ni sifa mojawapo inayowafanya wawe na rekodi nzuri katika ngumi za kulipwa hapa nchini.
Akizungumzia pambano hilo Ibrahim Kamwe kwa niaba ya muandaaji mkuu Mwalim Hatibu anasema kuwa maandalizi yamekwenda vizuri na mpaka sasa hakuna tatizo lolote kwa mabondia hao watakaocheza pambano kuu. Mapambano ya utangulizi ni kati ya Fabian Lyimo atazipiga na Musa Sunga pambano la raund nane huku Bakari Ustadh atazipiga na Frank Zagarino, wakati huo huo Tasha Mjuaji na Rama Johncena watatoana jasho.
Pia Yule bingwa wa PST uzito mdogo (minimum weight) goldsilver ataumana vikali na bondia kutoka klabu ya bigright boxing Herman Richard. Naye Ibrahim Kamwe anaongeza kwa kusema hilo, linaweza kuwa pambano kali sana la vunja jungu ambalo halijawahi kutokea kutokana na sifa na mabondia wenyewe na jinsi walivyo kamiana na uwezo mzuri wa kutupa makonde walionao