WADAU wa mchezo wa masumbwi nchini Tanzania wamejitokeza kuwa walinzi wa mapambano ya ngumi yalioandaliwa na promota Ally Mwazoa yatakayoanza Machi 29, Aprili 26 na Mei Mosi, 2014 katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam. Akizungumzia mpambano wa Japhert Kaseba na Thomas Mashali Mwazoa alisema maandalizi ya mpambano huo yamekamilika hivyo kinachongojewa ni siku na muda wa mpambano ufike.
Mwazoa alitoa shukrani kwa wadau ambao wamejitokeza kwa ajili ya ulinzi wa ali ya juu utakaofanyika siku hiyo kwa mabondia na wadau wengine watakaojitokeza. Aliongeza kuwa wapo wadau ambao wamekubali kulipa kiingilio na wameahidi pia kufanya ulinzi wa kila kona katika ukumbi huo. Alisema klabu mbalimbali za ngumi kutoka Wilaya za Temeke Ilala, Kinondoni, Mkoa wa Tanga pamoja na mikoa ya jirani wamejitokeza na kuthibitisha hakuta kuwa na fujo ambazo zitajitokeza siku kwa wale ambao wamejipanga kufanya fujo kwani ulinzi ni wa uhakika siku hiyo. Aliongeza kwamba kutakuwa na askari kanzu mbalimbali ambao watasaidia kudhibiti vurugu.
Mwazoa aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na kamera maalumu zitakazofungwa kila pande za kumbi ili kuona matukio mbalimbali ya nje na ndani yatakayokuwa yakiendelea na hata kudhibiti vitendo vya uhuzwaji wa tiketi feki na uingiaji kiholela na kusababisha usumbufu kwa wengine.
Akifafanua zaidi alisema siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi makali ambapo bondia Haji Juma atavaana na Juma Fundi wakati Fred Sayuni atapambana na Rajabu Mahoja na Zuber Kitandula atamenyana na Issa Omar wakati Bakari Dunda ataoneshana ubabe na Baina Mazola Mwazoa.
Aliwata wapenzi wa masumbwi kumiminika kwa wingi maana ulizi na usalama wa mali zako ni wa uhakika hivyo familia nzima mnaweza kuja kushudia mpambano huo wa masumbwi bila shaka