Movemba: Kampeni ya Mwamko Dhidi ya Kansa ya Tezi Dume

Dk Prathap C. Reddy

Dk Prathap C. Reddy

KATIKA mwezi wa Novemba kila mwaka jumuiya za kimataifa huadhimisha tukio ambalo hujulikana kama Movemba. Kampeni hiyo inahusisha kukuza kwa masharubu, kukusanya fedha na kuleta mwamko na ufahamu wa masuala ya afya kwa wanaume kama vile kansa ya tezi dume, kansa ya pumbu na saratani nyingine nyingi zinazowapata wanaume. Jina hiloni mchanganyiko wa neno “masharubu” na “Novemba”. Kampeni hiyo ya mwezi mzima inalenga katika kuongeza ufahamu na mwamko kwa kupima ili kugundua mapema kansa, utambuzi na matibabu ya ufanisi kwa lengo la kupunguza idadi ya vifo na hatimaye kuzuilika kabisa.

Mwaka jana peke yake zaidi ya dola milioni 120 zilikusanywa. Hadi sasa, Movemba imekusanya zaidi ya dola za marekani $ 550,000,000 kupitia wanachama wake milioni 4 katika nchi 21 duniani kote. Kampeni hiyo imefadhili zaidi ya dola milioni 25 na kuleta matokeo makubwa sana katika utafiti wa kansa ya tezi dume nchini Marekani.

Kansa ya tezi dume imekuwa mada moto mwezi huu nchini Tanzania kama kwingineko duniani limebaki kuwa tatizo kubwa. Licha ya Movemba kuchukua hatua ya kuleta muhamuko na ufahamu juu ya ugonjwa huo toka mwaka 2004, dhana uhamasishaji bado haijatiliwa mkazo kwa watanzania. Kansa ya tezidume ni muuaji wa kimya miongoni mwa watu wengi wa Tanzania na ni hali ambayo inahitajika kuletwa kwenye mwanga zaidi. Wanaume wengi wameendelea kuangukia mawindo kwa ugonjwa huu unaoongezeka kwa kasi ya hali ya juu kila sekunde, dakika na kila siku. Inakadiriwa kuwa watu wawili kila dakika tano hugundulika kuwa na kansa ya tezi dume duniani.

Kulingana nautafiti uliofanywa Januari 2014 na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORIC). Data zilizokusanywa kutoka kutoka mwaka 2006 zinaonyesha kuwa kila mwaka kumekuwa na ongezeko la kesi mpya ya wagonjwa kansa ya tezi dume. Katika mwaka 2013 idadi ya kesi mpya kuhudhuria taasisi ilifikia 115 kutoka 51 mwaka 2006 (i). Picha zaidi inaonyeshwa na utafiti wa mwaka 2011uliofanywa na Tanzania Cancer Registry mkoa wa Dar es Salaam, matokeo ya zoezi hili yalithibitisha kuwa kansa ya tezidume inaongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa kiume.
(ii)
Waziri Mstaafu wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa Homeli hapo awali alinukuliwa akisema “10% ya wagonjwa wanaosumbuliwa na aina mbalimbali za saratani wamejitokeza hospitalini kwa uchunguzi na matibabu. Iliyobaki 90% hawajafanya jitihada zozote kuhudhuria uchunguzi na matibabu.
Akizungumzia juu ya uchunguzi wa hali ya tezi dume nchini Tanzania, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Hospitaliya Apollo yenye makao makuu nchini India, Dk Prathap C. Reddy alisema kuwa “ugonjwa unaathiri watu wengi na kusababisha vifo vingi nchini kwa sababu ya ukosefu wa ufahamu wa kina juu ya ugonjwa huo. Utaratibu wa uchunguzi wa saratani ya tezi dume haufanyiki kutokana na gharama na ukosefu vifaa vya uchunguzi nchini.
Watu wengi hurejea hospitali wakati ugonjwa huo upo katika hatua ya mwisho, nahauwezi kuzuilika tena. Hata hivyo, ugonjwa huo una uwezekanomkubwa wa kutibika endapo utagundulika mapema. ”
Pamoja na kuwepo kifaa maalum cha utambuzi wa kansa ya tezi dume chaprostate specific antigen (PSA) duniani, Watanzania wachache sana wana uwezo wa kupata huduma hii. Kwa sababu kifaa hikikina gharama kubwa, na kinahitaji wafanyakazi wenye ujuzi na upimaji wenyewe ni gharama kubwa.
Mchungaji Dk Emmanuel Kandusi aliyenusurika na kansa ya tezi dume ana uzoefu wa kutosha juu ya ugonjwa huu na anajaribu kujenga ufahamu na uelewa kwa wananchi wenzake. Na pia nimwanzilishi wa 50 Plus Kampeni nchini Tanzania mara tu aliporejea kutoka kwenye matibabu nchini India. Haja ya kuanza kampeni zake mwenyewe dhidi ya kansa ya tezi dume nchini Tanzania inalenga kupunguza mateso na vifo vinavosababishwa na kansa ya Tezi dume.

Profesa David Mwakyusa

Profesa David Mwakyusa


Tofauti na watanzania wengi Rev Dk Emmanuel Kandusi alikuwa na uwezo wa kupata matibabu ushauri kutoka nje ya nchi. Wakati wa ugonjwa wake alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Apollo nchini India. Kutokana na maendeleo na upatikanaji wa vifaa muhimu na wafanyakazi wa kutosha katika hospital hiyo alikuwa na uwezo wa kuokoa maisha yake na kuanza kuwaelimisha wengine.

Hospitali za Saratani za Apollo, Hyderabad ni miongoni mwa hospitali zinazoongozaa kwa kutoa huduma na matibabu madhubuti za saratani. Hosipitali zinatoa matibabu ya mionzi, upasuaji kwa vifaa vya kisasa ikiwemo PET CT Scanner, NovalisTx ambacho ni kifaa kilichoundwa kwa ajili ya kuondoa vimbe zitokanazo na saratani mwilini. Hali kadhalika, hospitali hiyo inatoa fursa kwa wataalumu wake kujadili na kushirikiana katika kutafuta njia na tiba mbadala kwa wagonjwa saratani. Kwa sababu ugunduzi wa mapema wa ugonjwa wa saratani ni muhimu ili kutoa matibabu madhubuti, hospitali za Apollo zinatoa aina hii ya huduma hiyo ili wagonjwa wasichelewe kugundulika na saratani yamkini iliyoko katika hatua hatari za mwisho. Zaidi, huduma hizo zinatoa uchunguzi wa kitaalamu kwa jinsia zote hususan saratani ya tezi dume.

Ukilinganisha mazingira yalioko katika hospitali ya Apollo na hali ya taasisi zetu za afya nchini hakuna uwiano; kwani hadi sasa nchi ina kituo kimoja tu tiba ya mionzi ya saratani yaani Kituo cha saratani cha Ocean Road cha jijijni Dar-es-Salaam. Kutokana na ripoti ya kituo cha saratani cha Ocean Road (ORIC), mahitaji ya wagonjwa wa saratani nchini haishabihi huduma za saratani (i). Kutokana na tatizo hili na ukweli kwamba Ocean Road hakiwezi kukidhi mahitaji yote ya wagonjwa wote wa aina mbali mbali za saratani, mathalan wagonjwa hulazimika kwenda kupata matibabu yao nchini India hususan kwenye hospitali za Apollo.

Saratani ya tezi dume ni aina ya saratani ambayo huanzia kwenye tezi za kibofu ya jinsia ya kiume itokanayo na ukuaji hafifu wa seli inayopelekea uvimbe katika tezi. Baada ya hapo seli za saratani husambaa kutoka kwenye tezi dume kwenda sehemu nyingine za mwili husuan katika mifupa na matezi ambayo husabaisha maumivu hasa katika kupitisha haja ndogo, wakati wa tendo la ndoa. Hii ni aina ya saratani ambayo hushambulia zaidi wanaume walio juu ya miaka 50.
Tafiti zilizofanyika hivi karibuni zinaonyesha kuwa wanaume walio chiini ya miaka 40 wana uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa 1 kati ya 100,000. Na kwa wanaume walio kati ya miaka 70 na 74 wako katika kupata saratani ya hiyo kwa 1,326 katika ya 100,000.

Hali kadhalika inakisiwa mwanaume mmoja kati ya 6 hupata saratani ya tezi dume katika maisha yao (American Cancer Society – ACS 2008) na kila mwaka kati ya wanaume wote wanaogundulika na saratani moja ya nne wana saratani ya tezi dume. Desmond Tutu anaelezea ugonjwa huu, Saratani ya tezi dume haina mipaka ya kijamii”. Kwa idadi ya watu duniani, katika maisha ya mwanaume huwa na asilimia 16 (1 in 6) ya kugundulika na saratani ya tezi dume na asilimia 3 (1 in 33) ya kifo kitokanacho na saratani hiyo inayoua mwanaume mmoja kwa kila dakika 13. Pia kwa wanaume wote wanaogundulika na saratani mbali mbali kila mwaka, 25 huwa na saratani ya tezi dume.
Wakati dalili za tezi dume ni dhahiri, dalili hizo ni paomja na matatizo katika mfumo wa haja ndogo (ikiwa ni maumivu, kwenda haja ndogo mara kwa mara hususan usiku na kushindwa kuistahimili kwa muda), matone ya damu kati haja ndogo, maumivu katika sehemu ya chini ya mgongo, upotevu wa hamu ya kula na kupungua uzito.

Ili kugundua saratani ya tezi dume, mgonjwa anahitaji uchunguzi wa kina katika njia yake ya haja ndogo ambako daktari hujaribu kuhisi uvimbe wowote utakao kuwa katika mfumo wa mkojo na matezi uchunguzi ambao hufuatiwa na vipimo vya damu kama mgonjwa atagundulika na uvimbe wa aina yoyote ili kugundua kama kuna aina yoyote ya kemikali ijulikanayo kwa kitaalamu kama prostate-specific antigen (PSA) zinaohusiana na saratani ya tezi. PSA huwepo kwa asilia kwenye mfumo wa damu lakini ikionekana kuwa ya kiasi kikubwa katika damu basi huashiria uwezekano mkubwa wa mtu kuwa na saratani ya tezi dume.

Hivyo ni muhimu kwa wanaume walio juu ya miak 50 kupata vipimo na uchunguzi kwa ajili ya saratani ya tezi dume angalau mara moja kwa mwaka kwa ajili ya afya zao kutokan na ukweli kwamba jinsi ugonjwa utakavyogundulika mapema ndivyo matibabu yatakavyoanza mapema na mgonjwa kupona mapema.

Miongoni mwa vipimo ambavyo vinaweza kugundua kwa haraka sarataniya tezi dume kwa haraka ni kipimo cha damu cha PSA (Prostate-Specific Antigen) na DRE (Digital Rectal Exam na vipimo vingine kama ultrasound na needle biopsy vinavyohakiki kwa ufasaha kuwa mtu ana aina hiyo ya saratani lakini hakuna kipimo kimoja mbadala kugundua saratani hiyo.

Hakuna tiba mbadala ya kutibu kabisa saratani ya tezi dume lakini jinsi ugonjwa utakavyokugundulika mapema ndivyo njia mbadala zitakapotumika kuzuia athari zaidi za saratani hii. Hospitali za Apollo zilizoko nchini India zinatoa angalizo kuwa wanaume wote walio na miaka juu ya 40 wanapaswa kufanyiwa uchunguzi kwa kipimo cha PSA kila mwaka ili kujua afya zao juu ya saratani ya tezi dume. Hali kadhalika, wapate vipimo vya DRE na MRI vya nyonga na mifupa.

Sababu hatarishi za saratani ya tezi dume inajumuisha miaka, historia ya familia, kabila, chakula, vinjwaji, uvutaji sigara, uzito, madawa na aina ya pili kisukari. Kwa sasa matibabu ya wanume wanaogundulika na saratani ya tezi dume nchini Tanzania sio madhubuti hivyo kunahitajika mikakati kabambe ya kupunguza na kusimamisha ongezeko la wagonjwa wa saratani. Changamoto zilizopo sio za serikali tu bali kwa wote ikiwemo sekta ya afya na wananchi kwa ujumla na ni jukumu la wote kutafuta na kufanya njia mbali mbali katika kutokomeza na kuleta uelewa juu ya saratani hii ikiwemo jitahada zile zinazofanywa tayari na kampeni ya Movember.