Mourinho Afukuzwa Chelsea, Pep Guardiola Apigiwa Upatu

_85536554_mourinho_dismay_getty
Kocha wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Jose Mourinho amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya tangu atue darajani.

The Blues walitwaa ubingwa wa Ligi ya kuu msimu uliopita lakini msimu huu upepo umekuwa kinyume, na wamo katika eneo la kushushwa daraja.

Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich kabla ya kutoa tamko rasmi ya kumwachisha kibarua.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 52 amekuwa Chelsea kwa kipindi cha pili, kilichoanza Juni 2013.
jose-mourinho-chelsea_3359730
Chelsea walimaliza alama nane mbele kileleni msimu uliopita na kutwaa taji pamoja na Kombe la Ligi lakini mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa mechi tisa kati ya 16 ligini kufikia sasa.
Mourinho alitia saini mkataba mpya wa miaka minne tarehe 7 Agosti mwaka huu na ndiye meneja aliyefanikiwa zaidi akiwa na Chelsea.

Alishinda mataji matatu ya Ligi ya kuu kipindi chake cha kwanza katika klabu hiyo kati ya 2004 na 2007.
Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos na miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi.