Mount Meru Marathoni 2016 Kufanyika June

1

Mashindano ya riadha yajulikanayo kama Mount Meru Marathon yanatarajia kufanyika Mwezi June Mwaka Huu jijini hapa kwa kushirikisha wanariadha kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumzi hilo Mratibu Mkuu wa mashindano hayo Alfred Nicolas alisema wakiwa kama waandaaji wanahitaji kuhakikisha wanariadha wa Tanzania wanakuwa wakishiriki mashindano kila mara ili kuwafanya kuwa tayari kwa Mashindano yoyote ndani na nje ya Taifa.

“ Tayari wanariadha wameanza maandalizi kuelekea mashindano hayo na mwaka huu zawadi zimeongezwa tofauti na mwaka uliopita, hii yote ni kutokana na kujali michezo katika taifa letu” aliongeza kusema Nicolas

2

Aliongeza kuwa mashindano hayo ya nusu marathon wameyagawa kulingana na makundi ya wanaridha ambao wapo wanariadha watakaoshiriki mashindano ya mbio ndefu na kundi la pili ni wale wanaoshiriki mashindano ya mbio fupi yaani ya kujifurahisha hasa wazee na watoto.

“Bado kuna changamoto ya kuwapata wanariadha wanawake hata ukiwapata wengi wanakuwa wa kushiriki mbio fupi, hivyo kuwapata ni hadi katika vyuo na shule, japo JKT, na jeshi la magereza na polisi ndio wanajitahidi kuzalisha wanariadha wanawake.

Mashindano ya mount Meru Marathoni ni mashindano ya wazi hivyo kila mtu kutoka ndani na nje ya Tanzania anaruhusiwa kushiriki huku ada ya kila mshiriki.