Moto Mkubwa Waua Watu Kadhaa London

Moto mkubwa ukiteketeza sehemu ya jengo la Grenfell Tower, London.

Moto mkubwa ukiteketeza sehemu ya jengo la Grenfell Tower, London.

Moto mkubwa ukiteketeza sehemu ya jengo la Grenfell Tower, London.

MOTO huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza majira ya saa 01:16, saa za Uingereza. Hata hivyo Idara ya wazima moto jijini London ilituma malori 40 ya kuzima moto huo. Watu kadha wamefariki baada ya moto mkubwa kuteketeza jengo refu usiku wa kuamkia leo mjini London.

Wazima moto bado wanakabiliana na moto huo katika jumba la Grenfell Tower, ambapo walioshudia walisema kuwa watu walikwama ndani, wakiitisha msaada. Zaidi ya watu 50 wanatibiwa hospitalini. Mwandishi wa BBC alisema kuwa kulikuwa na hofu kuwa jengo hilo lingeporomoka.
-BBC