MABONDIA Sadiq Momba na Baina Mazola wamesaini mkataba wa kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo Mkoa wa Pwani uzito kwa kg 59
Akizungumza wakati wa kutiliana saini kwa ajili ya mpambano huo promota Muhusini Sharif amesema ameamua kuwapambanisha mabondia hawo wanaotamba kwa sasa kwenye uzito uho kwa ajili ya kuleta chachu ya mchezo wa ngumi nchini.
Sadiq Momba ni bondia maarufu ambaye anakwenda sana nje ya nchi kwa ajili ya mapambano mbali mbali na amekuwa anafanya vizuri awapo nje, Hata hivyo mpambano wake wa mwisho nchini Thailand alipigwa kwa T.K.O ya raundi ya tatu na kurudi nyumbani hivyo anachohitaji ni ushindi na kupigana na mtu mwenye point za kutosha ili kumrudisha kileleni
Baina Mazola katika uzito wake yeye ni namba tatu katika boxrec nchini hivyo nae anataka kuwa zaidi ya bondia Momba na ndio anatishia amani katika uzito huo kwa sasa.
Bondia Mazola amesema kwa sasa yupo vizuri sana na anawaomba mashabiki zake kuwa na moli ya kwenda bagamoyo ambapo promota kafanya vizuri sana kupeleka mpambao huu huko, mabondia wote wawili wanana umarufu mkubwa