Mohammed Dewji: Ubunge Singida Sasa Basiiii…!

Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia wapiga kura wake kama ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimboni humo wakati wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.

Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia wapiga kura wake kama ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimboni humo wakati wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.

IMG_7558

Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia wapiga kura wake kama ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimboni humo wakati wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.

MBUNGE wa Singida mjini na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amesema hatagombea ubunge wa jimbo hilo tena baada ya kulitumikia kwa miaka 10 na kuwezesha maendeleo makubwa katika sekta ya elimu na afya.

Mbunge huyo alisema hayo akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa People’s Club (MB) wakati wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa jimbo.Katika utekelezaji huo ametumia shilingi bilioni 5.

Miradi hiyo ni pamoja na kusaidia kuongeza shule za sekondari kutoka mbili hadi 15, kuwapo kwa vituo vya afya na kupeleka shule watu wenye mazingira magumu elfu 15.

Alisema ametekeleza majukumu yake ya kusukuma maendeleo katika jimbo lake la uchaguzi kwa ushirikiano mkubwa na kufanikisha vipaumbele vya wakati huo ikiwamo elimu na Afya

Alisema kwamba kujiondoa kwake katika siasa za jimboni kunatokana na majukumu ya biashara zake kuwa makubwa pamoja na kutaka kuwa karibu na familia yake baada ya miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.

“Ukichukulia kuongezeka kwa-mvi kichwani, ukilinganisha wakati wa awamo ya kwanza, nafikiri ni busara sasa kutimiza majukumu haya ya familia ambayo niliyabania nafasi yake kwa kipindi cha miaka 10.

“Pia siyo siri kwamba majukumu ya biashara zangu yamebadilika katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. ukuaji wa biashara zangu umeambatana na kuongezeka kwa majukumu, hususan mahitaji ya muda zaidi.

Mtazamo huu wa kuipa biashara muda zaidi ni muhimu sana kwa sababu mafanikio yangu kwenye biashara ndiyo yaliyoni-wezesha kuwatumikia, na yatakayo-niwezesha kuendelea kuwatumikia wananchi wa Singida kwa vitendo.” alisema.

Akizungumzia sekta ya afya alisema wananchi wa Singida walifanikiwa kukabiliana vilivyo na ugonjwa hatari wa Malaria kwa kugawa vyandarua zaidi ya vyandarua 6000 kwa mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5.

“Kwa kusambaza vyandarua hivi, tulifanyikiwa kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa asilimia hamsini” alisema akishangiliwa.

Aidha alishirikiana na mamlaka husika kupambana na ugonjwa sugu wa mtoto wa jicho kwa kupeleka madaktari bingwa na kufanya kambi kwenye hospital ya mkoa, waliotoa huduma ya upasuaji wa jicho na kutoa miwani kwa zaidi ya wananchi 1,000.

“Tulifanikiwa kujenga wodi ya macho, ndani ya hospitali yetu ya mkoa. Tulifanikiwa kuchangia ujenzi, wa zahanati za Mungumaji, na Manga ambazo zimekamilika! na zahanati ya kijiji cha Ititi ambao bado ujenzi unaendelea.” alisema

Pamoja na ujenzi huo pia alielezea mafanikio ya kusaidia baiskeli kwa walemavu na kufunga solar panel, pamoja na majokofu ya kutunzia dawa, kwenye zahanati za Manga na Unyambwa!

Akifafanua zaidi katika sekta ya elimu alisema kwamba walijenga vyumba vya madarasa, kuweka matangi ya maji ya kuvunia maji ya mvua, vyoo, na kusambaza madawati katika shule mbali mbali za msingi na sekondari jimboni Singida mjini.

Aidha alichangia vitabu zaidi 1000, vya masomo ya sayansi na sanaa, kwa shule zetu zote, za serikali ndani ya manispaa, ya Singida na tulifanikiwa, kuwapeleka wanafunzi wa shule ya msingi Ukombozi kwenye ziara ya kujifunza bungeni.

Akizungumzia sekta ya maji walifanikiwa kuchimba visima viwili kwenye mtandao wa Suwasa na vingine 45 ndani ya baadhi ya vitongoji vyetu vya manispaa ya Singida.

Aidha alisema alifanikiwa kusukuma mradi wa visima 10, unaofadhiliwa na benki ya dunia, akisisitiza kuwa wakati akiingia mwaka 2005 upatikanaji wa maji safi na salama ulikua asilimia 23 na sasa upatikanaji wa maji umefikia asilimia 81.

Pia alisema amefanikiwa kuisukuma serikali, kujenga barabara za kiwango, cha changarawe ndani ya manispaa na kufanya manispaa kuwe na barabara zinazopitika kwa kipindi chote!

IMG_7530

Mkazi wa Singida mjini akimwomba Mbunge wake asiache ngazi kwa maana bado wanamuhitaji baada ya kutangaza kutogombea tena.

Akiwashukuru wananchi wa Singida alisema kwamba: “kuwatumikia ninyi imekuwa ni tunu kubwa sana niliyo-barikiwa katika kipindi hiki cha miaka 10, na najisikia kuwa nimependelewa kwa kujifunza mambo mengi yanayohusu Singida na uongozi bora, na hususan mapungufu yake, ikiwemo mimi mwenyewe.”

Alisema dhamira yake kwa wananchi haitokani na nafasi yangu kama mbunge ama mwanasiasa, akisisitiza kuwa dhamira yake ya uzaliwa inayotokana na mapenzi aliyonayo kwao na imani aliyonayo juu ya uwezo wa kuijenga Singida.

“Mapenzi yangu na imani yangu kwenu hayapimiki, na ninapenda kuwahakikishia leo kuwa, haya yatajitokeza katika njia nyingine nyingi tu.”

Alisema pamoja na kutokugombea katika muhula wa tatu, lengo lake kuu la kutumikia wananchi wa Singida linabaki pale pale.

“Naomba nitoe ahadi kwenu! nitaendelea kushirikiana, na kada wa CCM, mtakaomchagua, kwenye nafasi hii ya ubunge katika shughuli zote za maendeleo ya jimbo letu! kwani dhamira yangu, ya kushirikiana nanyi, kujiletea maendeleo, haikuwa lazima mimi niwe mbunge, bali ilitokana na mapenzi yangu, kwa Singida na watu wake! “

IMG_7549

Mwanamama huyu akiwa haamini macho yake huku machozi yakimlenga lenga baada ya kusikia Mbunge wake kutogombea tena ubunge wa jimbo la Singida mjini.

IMG_7533

Watoto hawa machozi yakiwalenga na kuonyesha huzuni baada ya kumsikia mbunge wao akitangaza kuachia ngazi jimbo la ubunge wa Singida mjini.

IMG_7533

IMG_7535

Wananchi wa Singida wakisikiliza hotuba ya mbunge wao.

IMG_7536

IMG_7567

Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na mkazi wa kijiji cha Kinyampembe kata ya Meria ambaye ni mlemavu wa macho na miguu aliyefahamika kwa jina moja tu la Kangariga wakati wa hafla ya mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka ya ubunge wake, ambapo aliitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena jimbo la Singida mjini jana katika viwanja vya People’s Club.

IMG_7402

Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akiingia jukwaani na dancers wake kuwapa burudani wananchi wa Singida mjini.

IMG_7588

Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akitumbuiza wananchi wa Singida mjini wakati wa mkutano mkubwa wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa jimbo hilo.

IMG_7428

Pichani juu na chini ni Diamond Platnumz na ma-dancers wake wakishambulia jukwaa.

IMG_7440

IMG_7445

Umati wa wananchi wa Singida ukiwa uchizika na burudani ya Diamond Platnumz.

IMG_7447

IMG_7453

Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote na dancers wake wakitia mbwembwe kwenye show ya kukata na shoka katika viwanja vya People’s Club, Singida mjini.

IMG_7454

Chibu Dangote akishambulia jukwaa na dancers wake.

IMG_7471

IMG_7476

IMG_7478

Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote katika hisia kali kuwapa raha maelfu ya wananchi wa Singida mjini.

IMG_7481

Umati wa maelfu ya wananchi wa Singida mjini uliokusanyika katika viwanja vya People’s Club kusikiliza taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya ubunge wa Mh. Mohammed Dewji.

IMG_7610

IMG_7617

IMG_7626

Vijana wakimshangilia Chibu Dangote.

IMG_7629

Kijana wa Singida mjini (mwenye vest) akiimba jukwaa moja na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote.

IMG_7642

IMG_7633

Ngolololo…cha ngololo now, show me how the do ngololo…Chibu Dangote akionyesha madoido yake kwa wananchi wa Singida mjini.

IMG_7645

Shangwe za wananchi wa Singida mjini.

IMG_7675

Chibu Dangote akiwapa mikono wakazi wa Singida mjini wakati akiwaaga mara baada ya kutumbuiza.

IMG_7712

Kijisehemu cha maelfu ya wakazi wa Singida mjini waliojitokeza katika mkutano uliotishwa na Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji ambaye amewaaga rasmi.