Mohammed Dewji ahaidi zawadi nono Simba

Na Mwandishi wetu

Mbunge Wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji Ameitakia Kila La Kheri Timu Ya Simba Katika Mchezo Wake Wa Kuwania Kufuzu Kwa Hatua Ya Makundi Katika Michuano Ya Klabu Bingwa Afrika Dhidi Ya Wydad Casablanca Ya Morocco.

Mh. Mo Amewaambia Simba Kuwa Yuko Pamoja Nao Katika Dua Akiwaombea Mafanikio Ili Waweze Kuvuka Kizingiti Kilichopo Mbele Yao Na Kuwapa Watanzania Furaha Kwa Kushinda Katika Mchezo Huo Utakaochezwa Juni 28 Mwaka Huu Mjini Cairo.

Amesema Kitendo Cha Rufaa Yao Kukubaliwa Huku Timu Ya Tp Mazembe Ikiondolewa Na Simba Kuendelea Ni Ishara Ya Nyota Njema, Hivyo Wasipoteze Nyota Hiyo Ambayo Tayari Imeshaanza Kung’aa Na Badala Yake Waing’arishe Zaidi Kwa Kuwaadhibu Wamorocco Hao.

Mo Amewataka Wachezaji Wa Simba Kuwa Na Ujasiri Na Kujiamini, Na Kuwataka Wakumbuke Kile Timu Ya Simba Ilichokifanya Katika Michuano Kama Hiyo Mwaka 2003 Kwa Kuwatoa Timu Ya Zamalek, Basi Warudie Kitendo Hicho Hicho Ili Historia Ya Simba Ijirudie Na Kuweka Heshima Katika Medani Ya Soka Tanzania Na Afrika Kwa Ujumla.

Aidha Ametaka Watanzania Wote Tuondoe Tofauti Za Usimba Na Uyanga Na Tushirikiane Pamoja Katika Kuiombea Simba Dua Ili Ishinde, Kwa Kuwa Ushindi Wa Simba Ni Wa Watanzania Wote Na Sio Wa Wana Msimbazi Peke Yao.

Kwa Upande Wake Amewaahidi Zawadi Nono Wachezaji Wa Simba Iwapo Watafanikisha Azma Ya Kuwaondoa Wydad Casablanca Katika Mchezo Huo Wa Mkondo Mmoja Utakaochezwa Kwenye Uwanja Huru.

“Mimi Kama Mohammed Dewji Kwa Niaba Ya Wananchi Wote Wapenda Soka Nawaahidi Donge Nono, Lakini Sita Litaja Mpaka Hapo Mtakapo Tupa Raha Watanzania Kwa Kurejea Na Ushindi”.

Mh. Dewji Ametaka Watanzania Wote Tutumie Mchezo Huu Wa Simba Na Wydad Casablanca Kama Kiunganishi Na Tuwe Wamoja, Kwani Michezo Ni Furaha, Michezo Ni Upendo, Michezo Ni Afya Na Michezo Hujenga Umoja.

Kila La Kheri Simba Nawatakieni Ushindi Mnono Katika Mchezo Wenu.

“Simba Funga Hiyo Casablanca Bao Nyingi Za Kutosha Uingie Hatua Ya Makundi” Alisema Mo.

Mungu Ibariki Simba Sc

Mungu Ibariki Tanzania.

Akhsanteni