Mobisol Yanufaisha Familia Elfu 30 na Umeme wa Jua
Kasi hii ya ongezeko la wateja wanaotumia umeme nishati ya jua kutoka kampuni hii inadhihirisha kuwa uwekezaji wake unaendana sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania za kupunguza tatizo la upatikanaji nishati ya umeme nchini.
Katika kuadhimisha mafanikio ya kufikisha idadi ya wateja 30,000 Mobisol imetoa msaada wa kuinganisha na umeme wa nishati ya jua zahanati ya serikali ya kijiji cha Ngasamo kilichopo Simiyu ambapo anatokea mteja aliyejiunganisha na umeme wa kampuni hiyo akiwa anakamilisha idadi ya wateja 30,000 katika nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda ambako inatoa huduma zake.
Akiongea wakati wahafla ya kutoa msaada huo iliyofanyika katika zahanati hiyo,Meneja Masoko wa Mobisol, bwana Nkora Nkoranigwa amesema kuwa kampuni hiyo imejizatiti kuondoa tatizo la giza nchini na kuaikisha iawapatia wananchi umeme wa nishati ya jua wa uhakika kwa kutumia teknolojia ya kisasa na gharama nafuu.
“Sote tunaelewa kuwa nishati ya umeme inahitajika katika kuleta maendeleo ya haraka na kuwaongezea vipato hususani wakazi wa vijijini.Tutahakikikisa tunaunga mkono jitihada za serikali za kuzalisha na kusambaza umeme kwa kwa wananchi hususani wanaoisi maeneo ya vijijini kwa gharama nafuu ii uwasaidia katika itihada zao za kujiendelea kimaisha”. Alisema
Bwana Nkoranigwa Alisema umeme ikipatikana utasaidia wananchi kuachana na matumizi ya vibatari na kufurahia matumizi ya vifaa vya kisasa kama jokofu, feni, kuchaji simu na viginevyo na kuwezesha watoto kujisomea katika mazingira mazuri wawapo majumbani na mashuleni hali ambayo itasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika masomo yao.
Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Bwana Patrick Onyango alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa utawaondolea kero ya kukosa nishati ya umeme waliokuwa nayo kwa muda mrefu na itarahisisha utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa na aliahidi kuwa watahakikisha wanatunza vizuri vifaa vya nishati hiyo walivyozawadiwa “Kuna msemo kuwa akufaaye kwa dhiki ndio rafiki wa kweli”. Tunaishukuru kampuni ya Mobisol kwa msaada huu wa kusaidia wananchi wengi”Alisema.
Naye Afisa Utawala wa Wilaya hiyo Bwana Rabani Mageja kwa niaba ya serikali alishukuru kwa zahanati hiyo kupatiwa msaada wa nishati na aliongeza kuwa serikali wilayani humo itazidi kuunga mkono wawekezaji wanaokuja na miradi ya kusaidia kuleta maendeleo katika jamii kama ulivyo mradi wa nishati wa Mobisol.
Kwa upande wake mteja wa 30,000 wa kampuni ya Mobisol ambaye alisababisha hafla hiyo kufanyika kijijini hapo na zahanati kupatiwa msaada Bwana Kichoro alisema kuwa amefurahi kuona kampuni imemuenzi kwa kuleta msaada wa nishati kwenye zahanati wa kuwanufaisha wananchi wote.
Akiwa ni mteja wa umeme unaozalishwa na kampuni hiyo alisema ni wa uhakika na gharama nafuu na unafanya maisha kuwa rahisi na kisasa na kuwataka wanakijiji wajiunge kwa aili ya kuishi maisha ya kisasa na kuweza kuanzisha miradi midogo midogo ya uzalishaji kwa utumia nishati hiyo.