DAWASCO Kuzima Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini

KUZIMWA KWA MTAMBO WA MAJI WA RUVU CHINI
SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO),  LINAWATANGAZIA  WAKAZI WA JIJI LA DAR-ES-SALAAM NA MJI WA BAGAMOYO MKOANI PWANI  KUWA, MTAMBO WA KUZALISHA MAJI
WA RUVU CHINI UTAZIMWA  KWA SAA 36 KWA SIKU YA ALHAMIS TAREHE 18.02.2016.
 
KUZIMWA KWA MTAMBO HUO KUMETOKANA NA MATENGENEZO KATIKA BOMBA KUU LENYE UKUBWA WA INCHI
54 LINALOSAFIRI MAJI KUTOKA BAGAMOYO MPAKA KWENYE MATENKI YA MAJI YALIYOPO CHUO KIKUU ARDHI . 
MATENGENEZO HAYO YATAFANYIKA ENEO LA LUGALO JESHINI NA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI YA TAREHE 18/02/2016
 
 KWASABABU HIYO MAENEO YAFUATAYO YATAKOSA MAJI: MJI WA BAGAMOYO, VIJIJI VYA MAPINGA, KEREGE NA
MAPUNGA. BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.
 
MAENEO MENGINE NI MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, MANZESE, MABIBO, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.      
 
WASILIANA NASI KUPITIA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022-2194800 AU 0800110064
 
DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU
UTAKAOJITOKEZA
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
“DAWASCO TUTAKUFIKIA”.