MBUNGE wa Jimbo la Ubungo kupitia CHADEMA, John Mnyika ameshinda rufani iliyokuwa imewasilishwa na aliyekuwa mpinzani wake katika ugombea ubunge wa jimbo hilo, Hawa Nghumbi wa CCM. Mnyika ameshinda rufani hiyo baada ya Nghumbi kufuta rufani hiyo leo. Kwa mantiki hiyo sasa Mnyika anatambulika mbunge asiye na pingamizi hadi hapo utakapofanyika uchaguzi mwingine.
Tayari Mnyika amewashukuru wananchi wote waliokuwa naye pamoja katika kipindi chote cha mvutano wa kesi yake na Nghumbi. “Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kila mtu kwa nafasi tofauti iwe kwa sala, matashi mema, kuungana nami mahakamani, salamu kwa kheri kwa njia ya simu, SMS, humu Facebook, na mitandao mingine nk. Asanteni sana!! Mshikamano mlioonyesha uzidi kudumu katika jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo ndani ya Jimbo la Ubungo na nchi kwa ujumla. Nawaahidi kuendelea kuwatumikia na kuwawakilisha. Pamoja Tunaweza!!,” hii ni kauli ya mbunge Mnyika kwa wananchi mara baada ya kumalizika kwa kesi yake.