BAO la kipindi cha pili la mshambuliai Mrundi, Laudit Mavuto limeipa Simba SC ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo.
Mavugo alifunga bao hilo lililowaamsha vitini mashabiki wa Simba SC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam dakika ya tatu tu baada ya kuanza kipindi cha pili, akimalizia pasi ya Ibrahim Hajib.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Ruvu wakitangulia kabla ya Simba kusawazisha
Ruvu walianza kupata bao lililofungwa na Abulrahman Mussa dakika ya saba akimalizia pasi ya Fully Maganga, kabla ya Simba SC kusawazisha kupitia kwa Ibrahim Hajib aliyemalizia krosi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ dakika ya 11.
Katika kipindi hicho kila timu iliweza kufanya mashambulizi makali, huku Simba kupitia mchezaji Laudit Mavugo, akikosa nafasi tatu za wazi, katika dakika 19, 23 na 37 kwa kutokuwa makini.
Hajib naye akapoteza nafasi dakika ya saba na Kichuya dakika ya 21, kwa upande wa Ruvu Said Wigenge, akiwa yeye na kipa Vincent Angban alipiga shuti kali juu ya lango dakika ya 25.
Kiungo wa Ndanda, Jabir Aziz alitolewa kwa kadi nyekundu nyekundu dakika ya 79 baada ya kumchezea rafu kiungo wa Simba SC, Muzamil Yassin.
Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha Ndanda FC pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, awali ikishinda 3-1 dhidi ya Ndanda FC na baadaye kulazimishwa sare ya 0-0 na JKT Ruvu.
Michezo mingine ya Ligi Kuu leo, Yanga SC imelazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, wakati bao pelee la Muivory Coast, Kipre Balou limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Malika Ndeule, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Jamal Mnyate dk80, Said Ndemla/Muzamil Yassin dk71, Laudit Mavugo/Frederick Blagnon dk64, Ibrahim Hajib na Mwinyi Kazimoto.
Ruvu Shooting: Abdallah Rashid, Damas Makwaya, Mau Bofu, Frank Msese, Shaibu Nayopa, Jabir Aziz, Abulrahman Mussa/Baraka Mtuwi dk51, Shaaban Kisiga, Said Dilunga, Fully Maganga na Claide Wigengea
Chanzo: binzubeiry.co.tz