TAARIFA za mwendelezo wa tukio la mlipuko wa kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu katika Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi zinasema mtu mmoja tayari amefariki dunia huku zaidi ya majeruhi 30 wakiendelea kutibiwa katika hospitali mbalimbali Mkoani Hapa kufuatia mlipuko huo.
Baadhi ya majina yaliyotajwa hadi sasa ya majeruhi ni pamoja na Vovalt John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, John Thadei, Regina Fredirik, Joram Kisera, Novelt John, Rose Pius, John James, Anna Kessy, Joan Temba, Neema Kihisu, Regina Fredirik, na Joram Kisela.
Majeruhi wengine ni pamoja na Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim, Lioba Osward, Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga. Majeruhi wengi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru na Hospitali Teule ya St. Elizabeth.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo kuwa watulivu kipindi hiki na kuviachia vyombo vya usalama kuchunguza ili kuwabaini wahusika ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa pale inapobidi kufanikisha uchunguzi.
Aidha ameomba msaada wa madaktari wa ziada kwa haraka kuwahudumia majeruhi kwani wengine wamejeruhiwa vibaya. “Tunatakiwa kuachia vyombo vya usalama pekee tuwe watulivu na tutoe taarifa kwa Polisi lakini pia tunaomba msaada wa madaktari wa ziada katika hospitali kwani hawa majerui wameumia vibaya sana,” alisema Magesa.
Hadi sasa mtu mmoja amefariki dunia na zaidi ya majeruhi 50 wamegundulika kudhurika katika mlipuko huo. Majira ya saa nne asubuhi leo katika sherehe za uzinduzi wa Kanisa Kanisa jipya Katoliki la St. Joseph Mfanyakazi, hafla iliyokuwa ikiongozwa na Balozi wa Vatican nchini, Fransisco Padika na askofu Lebulu kumetokea mlipuko wa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu kilichorushwa na mtu asiyejulikana.