Na Said Mwishehe
MMILIKI wa Chama Cha Jamii(CCJ) Richard Kiyabo ameamua
kuvunja ukimya na kutaja majina ya waalinzishi wa chama
hicho huku akitumia nafasi hiyo kumshambulia kada wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Fred
Mpendazoe kuwa anatabia ya kukurupuka na kumtaka aache
siasa za udaku.
Amesisitiza kitendo cha Mpandazoe kumtaja Katibu wa
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi
Dk. Harrison Mwakyembe kuwa ni waanzilishi wa CCJ ni
jambo linaloshangaza na kwamba Mpandazoe amejivunjia
heshima aliyokuwa nayo kwa Watanzania.
Pia CCM Mkoa wa Dar es Salaam,imeitak CHADEMA nayo
kujivua gamba la ukabila kutokana na kuwa na wabunge
wengi wa viti maalumu kutoka Kanda ya Kaskazini huku pia
wakitakiwa kujibu hoja za Nape na hasa kuhusu mshahara
wa sh.milioni 7.5 anazolipwa Katibu Mkuu willibrod Slaa
wakati.
Akizungumza Dar es Salaam jana, kuhusu waanzilishi na
wamiliki wa CCJ, mmiliki huyo ambaye pia ndio alikuwa
Mwenyekiti wa CCJ, Kiyabo alisema kuwa chama hicho
kilianzishwa na yeye na Katibu Mkuu wake Renatus Muabhi
na ndio walikuwa wanahusika na kila kitu kuhusu
uuanzishwaji wa CCJ na hakuna mwanasiasa mwengine zaidi
yao.
Alisema hata katika usajili wa chama hicho kwa Msajili
wa Vyama vya Siasa John Tendwa majina yaliyopo ni ya
watu wawili ambapo ni yeye na Muabhi na kwamba hakuna
jina la Sitt, Mwakyembe wala Nape kama anavyodai
Mpandazoe ambaye naye alijuunga baada ya chama hicho
kuanza.
“Wakati CCJ inaanza mimi ndio nilikuwa nafanya kila kitu
kwa kushirikiana na Muabhi ambaye ndio alikuwa Katibu
Mkuu wa CCJ. Wakati tunaanzisha CCJ nachokumbuka Nape
alikuwa masomoni India. Hivyo miongoni mwa waliojiunga
nasi ni Mpandazoe ambapo baada ya kujiunga alitaka awe
mwenyekiti tukamkatilia na kwa kumpa heshima akawa
msemaji wa chama,” alisema Kiyabo.
Alifafanua kuwa wakati CCJ inaanza haikuwahi kuwa na
Sitta, Mwakyembe wala Sitta hivyo anachokisema Mpandazoe
ni kutoa kauli za uzhushi na zilijaa uongo mtupu na
kukurupuka ni kawaida yake ndio maana aliweza kukuruka
kwa kumkimbia mkewe Rose na watoto wake na kisha
kukimbia CCM na jimbo lake la Kishapu.
“Mpendazoe anadai kuwa waheshimiwa hao walikuwa ni
waanzilishi wa CCJ, hoja hiyo ni ya utata mkubwa.Swali
la kuuliza Mpendazoe wakati anaondoka CCM na kujiunga
CCJ alipokelewa na nani kati ya haoo anaowataja?
Walikuwa na nyadhifa zipi na namba za kadi zao za
uanachama.Je amesahau kuwa yeye alinukuliwa na vyombo
vya habari akimkaribisha Sitta CCJ,” alisema Kiyabo.
Aliongeza kuwa Mpandazoe hana hoja ya msingi kuhusu
kauli ambazo anazitoa na waanzilishi wa CCJ ambayo hivi
sasa ni marehemu kwa kuwa ilishakufa muda mrefu na
kuanzishwa kwa CCK na kumfananisha Mpendazoe kuwa hana
tofauti na mwanasiasa mdakuwa wa kisiasa yeye na chama
chake na kwamba wasidhani hiyo ni sera itakayowafikisha
Ikulu.
Kiyabo alisema kuwa anamshauri Mpendazoe na wenzake wa
CHADEMA waache siasa alizoziita za udaku na kwamba
Watanzania wanataka kusikia sera za chama husika na siyo
udaku. Wakiendelea na udaku wa kuwatuhumu watu kila
kukicha, mwisho wataanza kuamini pengine ndio sera yao.
Pia alisema hivi sasa CHADEMA inaonesha nguvu ya umma si
kura tena bali maandamano na vurugu zenye lengo la
kuitoa Serikali madarakani.Wao wanajiita chama cha
demokrasia na maendeleo lakini ajabu wanayoyafanya si ya
kidemokrasia bali ni chama cha maandamano na vurugu.