Mkwasa: Stars Yasasa Itakua si Mchezo

Mkwasa

Kocha Mkuu wa timu ya soka Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa Mei 18, 2016 atarajiwa kutangaza kikosi cha wachezaji wake wakaokwenda Kenya kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika jijini Nairobi, Mei 29, 2016.

Taifa Stars, itatumia mchezo huo utakaotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) katika rekodi zake, pia utatumiwa na kikosi cha Mkwasa kujiandaa dhidi Mapharao wa Misri katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (AFCON). Taifa Stars na Misri zinatarajiwa kuumana Juni 4, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.