Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mirajji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kufunga mafunzo
ya waendesha pikipiki.
Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha na kupunguza umasikini na kutunza mazingira nchini Tanzania (APEC), Respicius Timanywa akiwashukuru washiriki wote wa mafunzo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mirajji Jumanne Mtaturu akisisitiza juu ya umuhimu wa mafunzo ya usalama
barabarani.
Dc Mtaturu akionyesha kuku aliyokabidhiwa kama zawadi baada ya kukubali kuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo hayo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani wakionyesha alama za barabarani walizozichora wao wenyewe kwa ajili ya kuashiria kuelewa mafunzo waliyopatiwa
Baadhiya Bodaboda za washiriki zikiwa zimepaki bila kufanya kazi ya kubeba abiria ambapo wamiliki walikuwa kwenye mafunzo
Na Mathias Canal, Singida
SERIKALI imeeleza kuwa ipo tayari kuchukiwa na wananchi wavivu wasiotaka kujishughulisha na Ujasiriamali, Kilimo, Uvuvi, Ufugaji na Biashara ili kukuza pato la kaya zao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kufunga mafunzo ya usalama Barabarani kwa Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wa Wilaya ya Ikungi yaliyohusisha Kata ya Issuna na na Kata ya Mkiwa na kufanyika JMC Hotel Kijijini Issuna B.
Katika mafunzo hayo yaliyochukua siku sita yamewakutanisha pamoja waendesha Bodaboda 84 ambao wamefundishwa Alama na sheria zote za usalama Barabarani, Upatikanaji wa leseni, Faida za kulipa kodi na somo la ujasiriamali, Polisi jamii, Ulinzi shirikishi na elimu juu ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukosefu wa Kinga Mwilini (UKIMWI).
Akiwahutubia wananchi hao Mtaturu amemshukuru Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha ajira ya pikipiki kwani kwa kiasi kikubwa imesaidia kupunguza uhalifu na kuandaa ajira kwa vijana wengi nchini hivyo kuachana na kujihusisha na mambo yasiyo na tija kwa jamii ikiwemo kushinda vijiweni.
Amesema kuwa mafunzo hayo yanayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la APEC yatasaidia kupunguza ajali za pikipiki zinazosababishwa na uzembe wa baadhi ya waendesha pikipiki katika Wilaya zote za Mkoa wa Singida.
kuepusha ajali mpaka pale watakapopata mafunzo.
kusimamisha pikipiki sehemu isiyo rasmi jambo ambalo linachangia kuongezeka kwa ajali za barabarani.
kuwafanya vijana waweze kumiliki fursa kubwa na kutengeneza faida kubwa iliwaweze kulipa ushuru na kodi za serikali.