Mkuu wa Usalama Marekani Abwaga Manyanga..!

Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Usalama nchini Marekani, Julia Pierson.

Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Usalama nchini Marekani, Julia Pierson.

MKUU wa Idara ya Usalama nchini Marekani, Julia Pierson ambaye idara yake inahusika na kumlinda Rais wa nchi hiyo Barack Obama, ameamua kubwaga manyanga kazini baada ya shutuma kumzidia. Shutuma zilizokuwa zikimwandama zaidi ambayo huenda zimeshinikiza maamuzi ya kujiuzulu ni tukio la kuhatarisha usalama wa Ikulu ya nchini hiyo na taifa kiujumla.

Bi. Pierson alikabidhi barua ya kujiuzulu kwa Waziri wa Usalama wa Ndani tangu Oktoba Mosi. Hata hivyo siku moja kabla ya tukio hilo alikabiliana na maswali ya wajumbe wenye hasira kutoka Baraza la Congress juu ya udhaifu mkubwa wa usalama wa Ikulu ya Marekani.

Matukio yaliochochea maamuzi ya Bi. Pierson kujiuzulu ni pamoja na lile na mmoja wa askari wa zamani kuruka uzio wa Ikulu na kuingia ndani akiwa na kisu na lile la mtu mmoja mwenye silaha kuruhusiwa kuingia katika lifti moja na Rais Obama kulizidisha kutolewa wito wa kumtaka Mkuu huyo wa Usalama kujiuzulu.

“Leo, Julia Pierson, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Marekani, amenikabidhi barua ya kujiuzulu, na nimeikubali,” Waziri wa Usalama wa Taifa, Jeh Johnson aliandika katika taarifa yake. “Nampongeza kwa utumishi wake wa miaka 30 katika idara ya usalama wa taifa.” Alisema Waziri Johnson.

-BBC