Mkuu wa mkoa wa Singida atembelea Wizara ya Fedha Maonesho ya Nanenane Dodoma

Afisa uhusiano na Masoko wa Chuo cha Mipango Dodoma Godrick Ngoli (kulia) akimpa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kulia) jana ,jinsi Chuo hicho kinavyotarajia kutoa kozi mbalimbali zinahusu mazingira ili kukabiliana na changanoto ya ongezeko la watu haoa nchini . Mkuu huyo wa Mkoa alipata maelezo hayo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua jana mjini Dodoma kutoka kwa watendaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) kwanini kuna utofauti wa ubora katika bendera ya Taifa ya kuweka katika magari kwa viongozi. Mkuu Mkoa huyo aliuliza swali hilo jana alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma. Aliyeshika bendera ndogo ya taifa ni Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia).

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akitoa changamoto kwa watumishi wa Chuo cha Mipango cha Dodoma kuwa na mitaala ambayo itawaandaa wananchi kuanzia ngazi ya chini juu ya kuwa na mipango mizuri ya matumzi bora ya ardhi ili kukabiliana na ongezeko la watu nchini. Mkuu Mkoa huyo alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.

Picha na Tiganya Vincent, Dodoma