Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la kimataifa la OXFAM limezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mh Halima Dendegu na kuwataka washiriki kuuletea ushindi katika Mkoa wao wa Mtwara.
Halima Dendegu alitoa hamasa hiyo katika uzinduzi huo uliokwenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huku akiwataka washiriki ambao ni wanawake wajitahidi kadiri wawezavyo mshindi wa shindano hilo atokee mkoani mtwara.
Katika uzinduzi huo uliohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali, Taasisi za Umma, Mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wakazi wa Mkoa wa Mtwara pia Mh. Halima Dendegu alipata nafasi ya kugawa fomu za ushiriki kwa wakina mama watatu wa shindano hilo na kupata nafasi ya kuwaandikisha katika fomu hizo.
Pia katika hatua hiyo mkuu wa mkoa huyo amewaomba wakina mama wajasiriamali kujiokeza kwa wingi katika ushiriki wa shindano hilo ili kuongeza muamko wa shindano hilo na kujiongezea uwezo wa kushinda na kuwataka wanawake wajasiriamali kujaza fomu za ushiriki kwa wingi na bila ya kuogopa.
Sanjali na hatua hiyo mkuu wa mkoa amesema kuwa licha ya kuwepo na harakati za wanawake kujikwamua kiuchumi ambao wengi wao wanaotegemea kilimo kama njia ya kujipatia mazao lakini bado kumekuwepo na changamoto kubwa kwa mwanamke ya kumiliki Ardhi ambapo ametaja kama moja ya changamoto ya ukandamizaji wa kijinsia na kuwataka wanawake kusimama kidete katika kutetea haki hiyo kama moja wapo ya msingi.
Naye Meneja wa Utetezi wa Shirika la Kimataifa la OXFAM, Eluka Kibona alieleza kuwa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa mwaka huu 2016 linatarajiwa kuanza Septemba na litakuwa linaoneshwa kupitia kituo cha runinga cha ITV.
Meneja wa mradi kutokea shirika la OXFAM, Bi. Jovitha Mlay amewatoa hofu washiriki watakaoshiriki katika shindano hilo kwa kuwataka kujitokeza kwa wingi na hasa ikiwa kama bahati kwa shindano hilo la Mama shujaa wa chakula kuzinduliwa mkoani mtwara na hivyo kuwataka wakina mama wajasiriamali wakubwa na wadogo kujitokeza kwa kuchukua fomu za ushiriki kwa wingi.
Kamanda Mkuu wa Polisi Mkoa wa Lindi Renatha Mzinga akizungumzia nafasi ya Mwanamke katika kujenga Taifa wakati wa siku ya Maadhimisho ya Sikukuu ya wanawake Duniani.
Uzinduzi wa Mama shujaa wa chakula ulihudhuriwa na wasanii mbalimbali waliotoa burudani kwa wakazi waliofika katika uzinduzi wa shindano hilo; alikuwepo Valis Maembe, Mwasiti na Isha Mashauzi.Shindano la mama shujaa wa chakula lililoanzishwa na Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam lililoanzishwa hapa nchini mnamo mwaka 2011 lenye lengo zaidi ya kumsaidia mwanamke kujitambua zaidi katika haki zake mbalimbali na kujitambua kama mwanamke na kumuinua kiuchumi.