Mkutano wa wahariri Arusha waanza


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda aliyesimama akizungumza katika mkutano wa wahariri mjini Arusha jana. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini, Absalom Kibanda, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweriers (SBL), Jaji Marck Bomani, na wa kwanza kulia ni Katibu wa Jukwaa hilo ambaye pia ni mmoja wa wahariri wa magazeti ya Mwananchi Communication Ltd. Jaji Bomani alifungua rasmi mkutano huo jana mkoani Arusha, unaofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Kibo Palace. SBL imedhamini mkutano huo kwa gharama ya sh. milioni 168.