Kaimu Mganga wa Serikali, Dk.Donald Mbando wa pili kulia akijadiliana jambo na baadhi ya wadau wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu magonjwa yasiyopewa kipaumbele unaoendelea kwenye hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mganga wa Serikali, Dk.Donald Mbando wa kulia akisalimiana na mdau kutoka Shirika la Maendeleo la Misaada la Marekani (USAID), Dk. Angela Weaver katika mkutano mkuu wa mwaka wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu magonjwa yasiyopewa kipaumbele unaoendelea kwenye hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA MAGRETH KIANBO -MAELEZO).