Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Atembelea Clouds FM

Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon akisalimiana na mmoja wa watangazaji wa Clouds FM

 

Baada ya ziara kutembelea vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo, pia Steve Gannon alipata wasaa wa kukaa meza moja na uongozi wa juu wa kampuni hiyo na kuzungumza machache, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa ufanisi wa kikazi kwa mwaka mpya wa 2013. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga ‘Joe’ pichani kushoto akichanganua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Steve Gannon mara baada ya kutembezwa studio mpya na ya kisasa kabisa, iliyofungwa mjengoni humo, ambayo inatarajia kuanza kutumika hivi karibuni, Steve Gannon amefanya ziara fupi mwishoni mwa wiki na kutembelea vitengo vyote kampuni hiyo huku akijionea namna shughuli mbalimbali zinavyofanyika mjengoni humo.
Steve Gannon akitazama picha za wasanii mbalimbali wa nje waliowahi kufika nchini Tanzania na kufanya maonesho yao kadhaa ndani ya ofisi za Prime Time Promotions Ltd.

Mkurugenzi wa mambo ya utafiti na vipindi vya Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Steve Gannon ambaye nae alikuwa akimsikiliza kwa makini.

 

Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Steve Gannon akimuuliza jambo mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast, Gerald Hando kuhusiana na mambo mbalimbali ya kikazi, alipotembezwa kwenye studio ya ziada.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga ‘Joe’ pichani kushoto akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Steve Gannon mara baada ya kufanya ziara fupi mwishoni mwa wiki na kutembelea vitengo vyote kampuni hiyo huku akijionea namna shughuli mbalimbali zikifanya mjengoni humo.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Steve Gannon akizungumza jambo na baadhi ya wafanyakazi wa kitengo muhimu cha kampuni hiyo cha Masoko.
Steve Gannon akisalimiana na Oparesheni Meneja wa Prime Time Promotions Ltd. Balozi Kindamba, mara alipotembelea ndani ya kampuni hiyo ambayo imekuwa ikijihusisha na matamasha mbalimbali likiwemo tamasha kubwa la Fiesta ambalo hufanyika kila mwaka.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Steve Gannon akioneshwa matoleo mbalimbali ya jariba la burudani la KITANGOMA linachapishwa na kampuni ya Prime Time Promotions.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Steve Gannon akipeana mkono na Mmoja wa wafanyakazi wa Prime Time Promotions, Godliva Nicholaus mara alipowasili ndani ya ofisi za kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa mambo ya Masoko na Mauzo, Shebba Kusaga akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Steve Gannon.
Chief Editor wa Clouds TV, Bwa.Kanyopa akitoa maelezo mafupi kuhusiana na ufanyaji wao kazi ikiwemo na urushaji wa vipi kupitia Tv yao, Pichani kushoto ni Boss Joe akisikiliza kwa makini.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Steve Gannon alitembezwa pia ndani ya chumba maalum cha kuandalia habari, hapa Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Shaffih Dauda akifafanua jambo kwa Steve Gannon. Picha na JIACHIE BLOG.