Mkurugenzi Rombo Akiri Utoro Unawaangusha Kitaaluma

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya

Yohane Gervas, Rombo

UTORO na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati imetajwa kuwa ndio changamoto kubwa zinazoikabili Halmashauri ya Wilaya ya Rombo hali inayochangia ufaulu kwa wanafunzi kushuka.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya wakati alipokua akisoma risala kwa mgeni Rasmi katika sikukuu ya kilele ya maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa wilayani hapa. Mboya ameeleza sababu zinazopelekea utoro hasa kwa shule za ukanda wa chini ni biashara zinazofanywa maeneo ya mipakani.

“Mheshimiwa mgeni Rasmi moja ya sababu zinazochangia utoro ni biashara za mpakani na kupata mimba,” alisema Mboya.
Aidha amesema kuwa utoro huo unaanzia kwa wanafunzi wa darasa la nne hadi kidato cha nne.