Mkurugenzi Mtedaji Songwe Ageuka Mwalimu Ziarani, Aingia Darasani

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe Haji Mnasi akiwa darasani kufundisha wanafunzi huku wanafunzi wakiwa makini kusikiliza nini wanachofundishwa na Mkurugenzi hiyo.

 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe Haji Mnasi akiwa darasani kufundisha wanafunzi wa shule msingi alizotembea katika ziara yake.

Na Fredy Mgunda, Ileje

 
KATIKA hali isiyozoeleke kwa watumishi wengi wa Idara ya Elimu wilayani Ileje mkoani Songwe  kwa Mkurugenzi Mtedaji wa Halmsahauri ya wilaya hiyo kwa kuingia kwenye baadhi  ya shule za msingi na kufundisha.
 
Mkurugenzi huyo Ndugu Haji Mnasi ambaye kitaaluma ni mwalimu aliamua kufanya hivyo katika ziara  ya kushtukiza aliyoifanya kweye shule za Nyerere, Rungwa na Itumba zilizopo katika kata za Itumba na Isongole Tarafa ya Bulambya.
 
Akiwa katika shule ya Msingi Nyerere aliweza kufundisha masomo ya Kiingeriza, Hisabati na Kiswahili, pia aliweza kupima uelewa wa wanafunzi pamoja na kutoa maswali machache ya kuandika.
 
Ziara hiyo iliweza pia kumfikisha katika Shule ya Msingi Rungwa ambapo aliweza kuzungumza na walimu akiwapa moyo katika kuwapatia elimu bora wanafunzi akiwapa moyo wa utendaji kazi akiwataka kuzingatia  maagizo mbalimbali ya serikali.
 
Pia Mkurugenzi huyo,aliyekuwa amefuatana na mmoja wa viongozi wa Idara ya Elimu Msingi akiwa Rungwa aliweza kuzungumza na mafundi waliokuwa wakiendelea na ujenzi ambapo aliwataka kumaliza kazi kwa wakati wakifuata viwango vinavyotakiwa.
 
Ziara yake kwa siku hiyo ilishia katika shule ya Msingi Isongole ambako alipata fursaa kufuwatathimini wanafunzi wa Darasa la Saba ambao walikuwa wametoka kumalizia mtihani wa Moko ya Wilaya.
 
Mara baada ya kumalizia ufundishaji kwa masomo ya Hisabati,Kiswahili na Kiingereza Mkurugenzi huyo aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa jinsi walivyowaanda wanafunzi wao ambao wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Taifa siku chache zijazo.
 
Walimu kwa upande wao walimpongeza mwajiri wao kwa kuweza kutembelea shule yao na kuzungumza nao wakisema hali hiyo imewapaa ari ya kufanya kazi wakishauri ziara hiyo iendelee na kwa shule zingine
 
Mwalimu Denis Umbo alisema kuwa ,kitendo cha mwajili wao kuingia darasani hakijawatia moyo wa kufanya kazi tu bali ameitendea haki  taaluma yake na kujionea hali halisi ilivyo mashuleni badala ya kusubiri taarifa za mezani.
 
Si hayo tu yaliyojili katika shule hiyo pia Mkurugenzi  alibahatika kuzungumza na  wananchi waliokuwa kwenye mkutano  ambao pamoja na mambo mengine walitarajia kujadili masuala mbalimbali ya shule likiwemo la chakula cha mchana  kwa wanafunzi na taaluma.
 
Mnasi aliwataka wazazi hao kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu  ya Tano juu ya utoaji elimu bure kwa watoto wote hapa nchini.