MKURUGENZI wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds, Ruge Mutahaba amethibitisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia ofisi zao akiwa na askari wenye silaha. Akifafanua zaidi Ruge amesikitishwa na tukio hilo na kuviomba vyombo vya habari kuungana katika kupinga kitendo hicho cha uvamizi wa ofisi za vyombo vya habari pasipo utaratibu.
Alisema kitendo alichokifanya kiongozi huyo si cha kiungwana na matumizi mabaya ya madaraka jambo ambalo alitoi picha nzuri kwa mtawala. Alisema Clouds FM ni taasisi hivyo kulikua na kila njia ya kufanya kama imeenda kinyume na jambo lolote hivyo na si kuvamia kama ilivyofanya.
Aidha amethibitisha kuwa tukio la kuvamiwa Clouds TV na maaskari wenye bunduki kushinikiza kipindi kirushwe ni la kweli wala si tetesi kama ilivyokuwa ikidhaniwa na kudai awali walikuwa wakitafakari kwa muda kabla ya kuzungumza kama ingelitoka kauli ya kuomba radhi kwa kitendo kilichojitokeza.
Hata hivyo tayari waziri mwenye dhamana na habari Nape Nnauye amefika katika ofisi hizo kujua kilichotokea na huenda akalizungumzia suala hilo. Chini ni taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo kabla ya kutoa kauli leo.