Mkurugenzi Arusha Awatumbua Wawili Kituo cha Afya Kaloleni

Mkuu Wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Mkuu Wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

 

MKURUGENZI wa Jiji la Arusha, Athuman Kihamia amewasimamisha watumishi wawili wa kituo cha Afya cha Kaloleni kwa tuhuma za kutoweka kwa dawa na vitendanishi vya thamani ya shilingi milioni mbili. Kwa wa taarifa iliyotolewa na Afisa Tawala wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Frank Sanga waliosimamishwa ni Mfamasia Zephania Mtaturu na Msimamizi wa Maabara, Joyce Kitinye.

Katika maelezo ya awali watuhumiwa wamekiri kupotea kwa vitu hivyo na kuomba wavirejeshe mwisho wa mwezi jambo ambalo mkurugenzi hakukubaliana nalo. Alisema kitendo walichofanya ni wizi wa mali ya umma hivyo kuwataka wasimame kazi huku wakipisha uchunguzi wa tuhuma hizo.

Mkurugenzi ametaka ufanywe uchunguzi wa kina kwa vituo vya afya na zahanati nyingine kujua kama kuna matukio yaliotokea Kituo cha Afya Kaloleni.