Mkuchika awarejesha kazini madiwani waliotimuliwa Chadema

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za

Na Janeth Mushi, Arusha

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), George Mkuchika ameamuru madiwani wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliofukuzwa kuendelea na vikao na kulipwa posho zao hadi mahakama itakapotoa uamuzi juu ya kufukuzwa kwao.

Katika barua ya Mkuchika yenye kumbukumbu namba HA.23/235/01/06
iliyotolewa Agosti 23 na kumfikia Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,
Estomih Chang’ah imeeleza Wizara hiyo bado inawatambua madiwani hao na wataendelea kulipwa posho hadi hapo mahakama itakapotoa uamuzi
kama madiwani hao watano ni wanachama halali cha CHADEMA au la.

Madiwani hao na kata zao kwenye mabado ni, Estomii Mallah (Kimandolu), Ruben Ngowi (Themi), John Bayo( Elerai), Charles Mpanda( Kaloleni) na Diwani Viti Maalum, Rehema Mohamed, amesema kisheria wataendelea kuhudhuria vikao na kulipwa posho zao, hadi mahakama itakapotoa muamuzi wa mwisho hivyo ni vyema suala hilo likasubiriwa kutolewa maamuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Mkurugenzi wa
Manispaa ya Arusha, Chang’ah alisema amepokea barua hiyo hutoka kwa
Mkuchika ikitoa maelezo kutokana na barua ya awali ya aliyoindika MD/ US/101/ 1/107, Agosti 12 mwaka 2011 akiomba mwongozo juu ya suala hilo.

Alifafanua kuwa suala la madiwani hao kuendelea na nafasi zao litatokana na uamuzi wa mahakama kwani walishafungua kesi ya madai
hivyo mahakama ndio yenye kutoa uamuzi kisheria pia barua hiyo
imetolewa na nakala kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima,
Katibu Mkuu, Wilbroad Slaa pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Alisema katika Sheria ya Serikali za Mitaa namba 8 ya mwaka 1982
kifungu cha 26 (1) (e) kinafafanua kuwa Waziri mwenye dhamana na
Serikali za mitaa atatamka kuwa nafasi ya diwani iko wazi baada ya
kupokea taarifa rasmi ya maandishi kutoka kwa Mwenyekiti au Meya wa
Jiji la Arusha.

Alisema suala la kuambiwa kuwa anakumbatia madiani hao yeye kama
Mkurugenzi linamuuza kichwa na anapokea tuhuma nyingi juu ya madiwani hao pia maendeleo ya Jiji la Arusha hafanyiki kutokana na mgogoro huo na waziri ameshatolea ufafanuzi hivyo kutokana na uamuzi huo wa waziri busara zinahitajika zaidi.

Naye Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa amesema amewasilisha barua ya kuwavua uanachama madiwani hao kwa Mkurugenzi Agosti 8 mwaka huu na alipowasilisha kwa dispacha na kushangaa kuwa barua hiyo iliyotoka kwa Waziri wa Tamisemi ilimfikia Agosti 12 mwaka huu na si Agosti 10 kama
nukushi inavyoeleza.

Alisema suala la Arusha inabidi liangaliwe kwa kina kwani inavyoonekana wanapoteza muda wa maendeleo kwavitu vya kipuuuzi kwani wasipoangalia kuhusu maamuzi sahihi ya mgogoro wa Arusha kitakachotokea ni kama suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo la Rais kumsimamisha kazi huku Katibu Mkuu, Philemon Luhanjo akimtaka arudi kazini.

Alisema katiba ya Chadema inasema ukishavuliwa uanachama hutakiwi
kujihusisha na masuala ya kisiasa kwa sababu si mwanachama hivyo
madiwani hao wanalipwa posho za wananchi kwanini na wanahudhuria vikao vya Baraza la Madiwani wakati chama hakiwatambui wala mahakama
haijasikiliza kesi yao ya msingi waliyoifungua.

“Katiba ya CHADEMA inasema kuwa ni marufuku kwa masuala ya Chama
kupelekwa mahakamani masuala ya cahama ni ya chama na yeyote
atakayekwenda mahakamani atafukuzwa ndani ya Chama,” alisema Dk. Slaa.

Aliongeza kuwa inashangaza madiwani hao kufungua kesi mahakamani
wakatiw akiwa tayari wamekata rufaa Baraza Kuu la Chadema kuomba
warudishiwe uanachama.

Naye Mbunge wa Arusha, Godbless Lema alisema kutokana na madiwani hao kufungua kesi mahakamani na mahakama haiajatoa majibu kwanini madiwani hao waudhurie vikao na kupokea posho hivyo viongozi wasipoangalia suala hili kwa makini siku 30 walizozitoa kuhusu mgogoro wa Umeya Arusha hazitafika kwani CHADEMA hawawezi kuvumilia kodi za wananchi zikaliwa na wachache ambao wamevuliwa uanachama.