MJUKUU wa Mzee Nelson Mandela, Mandla Mandela ameshindwa kesi iliyowasilishwa mahakamani dhidi yake kwa tuhuma za kufukua makaburi ya jamaa za familia yake katika mzozo wa makaburi uliozua utata ndani ya familia ya Mandela.
Mgogoro huo unahusu maiti za wanawe Mandela watatu ambao Mandla alihamisha na kuwazika karibu na nyumbani kwake zaidi ya miaka miwili iliyopita. Taarifa zinasema Mahakama Kuu imeamuru kuwa maiti hao lazima warejeshwe katika makaburi yao Jumatano.
Wakati mzozo wa kesi hiyo ukiendelea mzee Mandela anaendelea kuugua hospitalini na haijulikani ikiwa mawakili wa Mandla wataka rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama au la.
Jamaa za familia ya Mandela waliwasilisha kesi ya uhalifu dhidi ya Mandla kwa kosa la uhalifu. Msemaji wa polisi, Mzukisi Fatyela aliviambia vyombo vya habari kuwa maofisa wa usalama watachunguza tuhuma dhidi ya Mandla za kufukua makaburi kinyume na sheria na ikibainika anakosa huenda akashtakiwa.
Inahusisha maiti za watoto watatu wa Mandela ambao inaaminika walifukuliwa na Mandla kutoka makaburi ya familia miaka miwili iliyopita. Familia ya Mandela, inataka kurejesha miili hiyo katika kijiji cha Qunu, ambako Mandela, ambaye anaumwa sana hospitalini anataka kuzikwa akifa.
Kesi hiyo iliyosikilizwa katika mahakama kuu ya Mthatha, katika mkoa wa Mashariki iliakhirishwa hapo jana lakini hukumu ikitaolewa Jumatano. Hivi karibuni mahakama ilitoa amri ya muda kwa maiti za watatu hao kuhamishwa kutoka nyumbani kwa Mandla katika Kijiji cha Mvezo hadi Qunu, umbali wa kilomita 22.
Lakini Mandla Mandela, ambaye alitawazwa kama kiongozi wa kijamii na babu yake, sasa alipinga vikali amri hiyo.
-BBC