Mitandao Inavyochochea ‘Rushwa’ ya Ngono

Aina mbalimbali ya mitandao ya kijamii

Aina mbalimbali ya mitandao ya kijamii

Matumizi ya kampyuta mpakato

Matumizi ya kampyuta mpakato


Na Mwandishi Wetu
WANANCHI kwa ujumla wanatakiwa kuwa makini na matumizi ya mitandao mbalimbali kwa kutumia simu zao za mkononi, kompyuta na vifaa vingine. Hii ni kutokana na baadhi ya watu kutumia mitandao vibaya kwa kuwatishia watu na hata kwa wizi kwa lengo la kujipatia kipato toka kwa marafiki wakaribu au wapenzi wao wa zamani kwa kuitaji kiasi kikubwa cha fedha ili kuweza kuwadhibiti wasiweze kutoa siri zao.
Kimsingi kuibuka kwa wimbi hili kunaifanya jamii kuwa makini kwa marafiki zao wa karibu kwani huweza kuwatisha na wakati mwingine husambaza picha mbaya kwenye mtandao wakishindwa kutimiza kutoa kiasi cha pesa wanachoitaji.
Pamoja na hayo bado jamii inaaswa kuwa makini na matumizi ya simu katika mtandao unaweza kusababishana rushwa ya ngono inaweza kutokea kwa kutumia mtandao kwa mfano mtu mpenzi wako wa zamani umeachana naye kwa bahati mbaya kwa kutokupenda aliwahi kukupiga picha za uchi na kudhifadhi kwenye simu mnapokorofishana ugeuka na kukukomesha kwa kukudhalirisha katika mtandao.
Aidha baadhi ya watu simu zao zinaibiwa na vibaka au wanadondosha barabarani hanaipata mtu ambaye nia yake si nzuri hana shida na pesa hivyo hufanya ndio njia mojawapo ya kuweza kujipatia kipato kwa kukutishia kuzisambaza picha zako ambazo sio nzuri ambazo umepiga ukiwa upo mtupu.
Matatizo mengine yanayotokana na ukatili wa kijinsia yanasababisha na mazingira ya kutumia mtandao na wakati mwingine mtu akishajua skendo yako mbaya au amekuchua video mlipokuwa wapenzi uwa ndio fimbo ya kukunyanyaswa, wakati mwingine utumia fursa hiyo kukulazimisha kufanya mapenzi kinguvu au kukufanyia ukatili wa kijinsia pale anapokuitaji na wewe kushindwa kumkatalia kwa kutokuwa na ujasiri wa kuweza kutatua tatizo lako.
Baadhi ya watu upata ujasiri wa kutoa taarifa kituo cha polisi kuhusu mpenzi wake wa zamani anavyomfanyia vitendo vya ukatili au wengine ukimbilia kwenye vyombo vya msaada wa kisheria kwa ajili ya ushauli.
Utafiti unaonesha kuna baadhi ya kesi mbalimbali za ukatili wa kijinsia zinalipotiwa kituo cha polisi kuhusu rushwa ya ngono kwa kupitia mtandao au picha za utupu ambazo husambaza kwenye internet bila ridhaa ya muhusika na baadhi ya watu ukamatwa wakiwa wanarekodi picha za watu kwa kutumia usiri kutegesha kwenye vyumba vya kulala wageni.
Hivyo basi jamii kwa ujumla tunaomba tuwe makini sana katika kutumia mitandao ya kijamii na kuelewa hasara zake zinaweza kusababisha ukatili wa kijinsia baadhi ya watu wakapoteza maisha kwa kuona picha mbaya za ndugu zao zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Pia jamii kwa ujumla tuwe wa kwanza kupinga rushwa ya ngono kwa kutumia mtandao na kuchua hatua ya kuelimishana na jirani yako athari za kutumia mtandao vibaya inaweza kusababisha rushwa ya ngono kuacha kuwasiliana na marafiki usiowajua kwenye mtandao na kuwatumia picha zako za utupu na picha za familiya yako bila kuonana nao ni mtu wa aina gani vilevile kuwa makini na matumizi ya mtandao ya kijamii kama vile twiter, instagram, what’sup, facebook na tango nk.
Tunaomba serikali na wizara yenye dhamana (TCRA) itoe mafunzo ya kutosha kwa watu wanaomiliki mitandao ya kijamii kama Tigo, Vodacom, Zantel, Airtel na kuweze kudhibiti usambazaji wa picha na video potofu kwa wanajamii na kuwakamata watu wanaofanya vitendo vya aina hii na kusababisha ukatili wa kijinsia kama rushwa ya ngono kwa kutumia mitandao ya kijamii.
Vilevile wanaharakati na wadau wengine kama chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA), CRC, TGNP, WIRAC, TAWLA, LHRC, TACOLTA, Vyombo vya sheria na wanajamii waweze kushirikiana kwa pamoja kutoa elimu ya kutosha kuhusu kupiga vita rushwa ya ngono katika mazingira ya kazi na katika mazingira ya mitandao ya jamii ili kunusulu maisha ya watu katika harakati za kupiga vita Ukatili wa kijinsia.