Mhifadhi katika Hifadhi ya Tarangire, Beatrice Kessy (kulia) akifafanua jambo kwa washiriki Miss Utalii Tanzania 2011, katika ziara yao.
BAADA ya kukamilisha uundaji mfumo mpya wa uongozi na uteuzi wa wakurugenzi 60 wa kamati ya Taifa hadi Wilaya wa Mashindano ya Miss Utalii Tanzania, bodi ya wakurugenzi ya Miss Tourism Tanzania Organisation, yenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo nchini, imeandaa semina elekezi kwa wakurugenzi wote wa Majimbo, Wilaya, Mikoa, Kanda, Kanda Maalum za Vyuo Vikuu na wa kamati ya Taifa.
Semina hiyo imepangwa kufanyika Ijumaa, tarehe 5, 2011 katika ukumbi wa hoteli ya Royal Village mkoani Dodoma. Semina hiyo elekezi ni sehemu ya mpango mkakati wa kuimarisha uongozi na kuboresha zaidi mashindano hayo, ambapo washiriki wata fundishwa juu ya kanuni na taratibu za mashindano ya Miss Utalii Tanzania, Utawala na Uongozi wa Mashindano ya Urembo, Utalii, Utamaduni, Uwekezaji, Mazingira, Uzalendo, Utalii wa Ndani, Utalii wa Kitamaduni, Umasikini, Afya ya Jamii, Hifadhi za Taifa, Hifadhi za Bahari, amani na Umoja.
Wakufunzi katika semina hiyo ni wadau na mamlaka husika katika kila mada na wajumbe wa bodi ya mashindano hayo.
Semina hiyo itafuatiwa na uzinduzi rasmi wa kuanza kwa msimu mpya wa Miss Utalii Tanzania 2011/2012 unao anzia 1-8-2011 hadi Mwezi Machi 2012 ambapo fainali za Taifa za Mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2011/12 zita fanyika. Semina na Uzinduzi huo zitahitimishwa kwa kufanyika kwa shindano la Miss Utalii Dodoma 2011/2012 katika ukumbi wa Royal Village Dodoma siku ya mkesha wa sherehe za 88 7-8-2011.
Pia siku hiyo utafanyika uzinduzi rasmi wa safari ya Kihistoria ya washindi wa Taifa wa Miss Utalii Tanzania 2010/2011 ya kutangaza Utalii, Utamaduni na kuhamasisha Utalii wa Ndani, Utalii wa Kitamaduni,vita dhidi ya uharibifu wa mazingira, Maradhi, Uvuvi haramu ,uwindaji haramu ,Tamaduni kongwe na potofu na pia kuhamasisha matumizi na kuthamini bidhaa za Tanzania.
Wakurugenzi wapya wa kamati ya taifa ni pamoja na Idrissa Mzilai, Grace Kihongozi, Abdalla Hamza Uweje, Violet Kaberege, Clifford Ndimbo, Richard Tusiime Buhembo, John Kalonga, Clemence Kambengwa, Joachim Mkwabi, Sophia Athumani Dio, Noel Shani, Rehema Salim, Yahya Mohamed Freddy Mwanjala, Godwin Gondwe, Pendaeli Omari, Baruani Mhuza, Simon Mkina, Daniel Mtanga, Frank Kananura, Mwasiti Ramadhani Gange, Francis .N. Mhando, Peter M. Kaiza, Samora Chokala, Dianna Henry, Amina Haruna, Joachim Mkwabi, Emanuel Manase, Dr. Emanuel Simbe, Zenna Ramadhani Gange, Francis Samuel, Faraja Mwella, Charles Gabriel ,Deissy Vedasto, Radio Five, na Emmanuel Masabo.
Miss Tourism Tanzania Symbol Of National Heritage – Do Value Added Pageant
“Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Lining”
Regard,
Gideon E.G. Chipungahelo
PRESIDENT / C.E.O
Hotline: + 255 – 715/754/773 – 318 278.