SHINDANO la kumsaka Miss Utalii Mkoa wa Kagera 2012, litafanyika katika Ukumbi wa Linas Club Julai 14, 2012 kuanzia saa, mbili usiku. Katika shindano hilo la mwaka huu warembo 15 watachuana kuwania taji la miss Utalii Tanzania 2012- Kagera.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandaaji wa onesho hilo kwa vyombo vya habari, washiriki watapita jukwaani katika mavazi ya kitanzania ya Ubunifu, kitalii, kutokea na ya asili, huku wakitangaza Utalii, Utamaduni, urembo wa kitalii, ubunifu na vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili za makabila ya Mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla.
Taarifa zaidi zinasema kuwa burudani mbalimbali za Ngoma za asili, bendi na wasanii wa muziki wa kizazi kipya watakuwepo, wakiwemo Diamond Musica Band, Agcox Burchaman toka Uganda, Maua na BK Sunday.
Shindano hilo limedhaminiwa na Cargo Star, Vodacom Tanzania, Kroyera Tours, Vission Radio, Kasibante Radio, prins Hotel, Paradise Hotel, Linas Club ,Mice and Lovely Salon,misstourismorganisation.blogspot.com na Amazing Tanzania Tours(Tours and Safaris).
Washindi wa shindano hilo watawakilisha mkoa wa Kagera katika fainali za miss Utalii Tanzania 2012- Kanda ya Magharibi, na baadae katika fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012 zitakazofanyika siku ya mkesha wa Uhuru wa Tanzania Desemba 8, 2012.
Miss Tourism Tanzania Symbol Of National Heritage – Do Value Added Pageant
“Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Lining”
Mawasiliano zaidi: + 255 – 715/754/773 – 318 278.
www.misstourismorganisation.blogspot.com