Miss East Africa 2012; Ethiopia yatoa mshiriki

Miss Lula Teklehaimanot

WAREMBO watakaoziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu wanaendelea kupatikana kutoka katika nchi mbalimbali zinazoshiriki mashindano hayo.

Mrembo mwingine aliyeingia fainali ni Miss Lula Teklehaimanot (19) kutoka nchini Ethiopia ambae alipatikana mwishoni mwa wiki baada ya kuwashinda warembo wenzake waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Ethiopia katika fainali hizo.

Miss Lula Teklehaimanot ana urefu wa meta 1.79 na uzito wa kilogramu 52 ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha St. Merry cha jijini Addis Ababa, Ethiopia ampapo anasomea Shahada ya Masoko. Pia mrembo huyo ni miongoni mwa wanamitindo maarufu wanaochipukia kwa kasi nchini Ethiopia.

Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika Septemba 07 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius. Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es Salaam.