Mikataba ya Kimataifa Iwe Sheria Kamili – TGNP Mtandao

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (aliyesimama) akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake nchini iliyoadhimishwa katika viwanja vya TGNP Mtandao leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake nchini iliyoadhimishwa katika viwanja vya TGNP Mtandao leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akisisitiza jambo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake nchini iliyoadhimishwa katika viwanja vya TGNP Mtandao.

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) Bi. Zuki Mihyo (aliyesimama) akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake nchini iliyoadhimishwa katika viwanja vya TGNP Mtandao leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) Bi. Zuki Mihyo (aliyesimama) akizungumza Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake nchini iliyoadhimishwa katika viwanja vya TGNP Mtandao leo jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake nchini iliyoadhimishwa katika viwanja vya TGNP Mtandao leo jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

WANAHARAKATI wa masuala ya haki na usawa wa Kijinsia nchini wamependekeza Bunge maalum la katiba kuhakikisha katiba mpya inaweka wazi kila mikataba ya kimataifa itakayoridhiwa iwe sheria kamili za nchi.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake nchini iliyoadhimishwa katika viwanja vya TGNP Mtandao leo Machi 5, 2014, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Bi. Lilian Liundi, amesema kuwa mchakato wa kuandikwa upya kwa katiba mpya ni fursa kwa Tanzania kuangalia upya suala la kuhakikisha mikataba ya kimataifa na kikanda inayoridhiwa inakuwa sheria kamili za ndani.

“Nchi yetu imeridhia mikataba mbalimbali ya kutetea haki za wanawake; kwetu sisi tunaona hii ni fursa hasa katika mchakato wa kuandika katiba mpya ambapo tunadai mikataba ikisharidhiwa / siiniwa iwe imeridhiwa nyumbani na iwe sheria moja kwa moja. Pia mikataba hiyo iwe shirikishi.” Alisema Liundi na kuongeza:

“Kumekuwa na ongezeko la nafasi za uongozi hasa katika bunge japokuwa bado katika nyanya nyingine bado tuko mbali sana ndio maana tuna dai kubwa la hamsini kwa hamsini katika nyanya zote za uongozi. Ukiangalia uwiano kijinsia bado kabisa. Baraza la mawaziri 27%; bunge 34%; makatibu wakuu 17.8%; makamishna wa tume mbali mbali 30.8%; wakuu wa mikoa 27%; wakuu wa wilaya 32%; madiwani wa kuchaguliwa 4%; wenyeviti wa vijiji 2%; wenyeviti wa mitaa 12% vitongoji 3% (Ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za Mitaa 2009)” aliongeza
Liundi alisema kuwa pamoja na ongezeko la shule za kata japokuwa bado hazikidhi mahitaji majengo yapo lakini walimu ni wachache na wengi hawana ujuzi wa kutosha, mabweni hakuna, umbali hii inasababisha mimba mashuleni hasa kwa wasichana. Alisema huduma za afya japo kuna vituo vingi vya afya lakini huduma hakuna, wahudumu, madawa. Nishati wanawake bado wanapikia kuni wanatumia muda mrefu sana kutafuta maji wanakosa muda wa kufanya shughuli za kiuchumi.
Akizungumzia kwa upande wa Uchumi amesema: “Bado bajeti yetu ya taifa haijaweza kuwa na mrengo wa kijinsia yaani kuangalia mahitaji ya makundi mbali mbali na kugawanya rasilimali kulingana na mahitaji hayo. Bado bajeti kubwa inaelekezwa katika njanya zinazowanufaisha watu wachache”.
Aidha amebainisha kuwa bajeti ya taifa bado ni tegemezi kutokana uchambuzi wa mwongozo wa bajeti 2014 bado 42% ya bajeti inategemea wafadhili.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) Bi. Zuki Mihyo, amesema kuwa kuna umuhimu mikubwa harakati za kudai usawa wa Kijinsia na ukombozi wa mwanamke kuenda sambamba na kujenga uwezo kwa wananchi hasa wanaharakati ngazi ya jamii.