Mifuko ya Bima Yatakiwa Kuwekeza Kwenye Viwanda

Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akizungumza na Wakurugenzi  na Watendaji wa Mifuko  ya Hifadhi ya Jamii katika mafunzo kwa bodi za udhamini za mifuko ya hifadhi ya jamii kuhusu uendeshaji na usimamizi wa mifuko ya hifadhi  yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mifuko ya hifadhi ya jamii (TSSA) yaliyofanyika jana jijini Arusha.Picha na Pamela Mollel

Na; Ferdinand Shayo,Arusha.

Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye viwanda ili kuchochea uchumi wa viwanda utakaolisaidia taifa kukua kiuchumi na pia kuwanufaisha wanachama wa mifuko hiyo kutokana na uwekezaji huo wenye tija.

Jenista Amesema hayo akizungumza na Wakurugenzi wa Mifuko pamoja na Watendaji katika mafunzo kwa bodi za udhamini za mifuko ya hifadhi ya jamii kuhusu uendeshaji na usimamizi wa mifuko ya hifadhi yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mifuko ya hifadhi ya jamii (ISSA) .

Amewataka Wakurugenzi hao kuunga mkono Agenda ya taifa ya kulifikisha taifa kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda.

Waziri huyo amewataka Wakurugenzi wa mifuko kuhakikisha kuwa wanadhibiti mifuko hiyo ili wanachama waweze kupata mafao yao kwa wakati muafaka bila kuwepo kwa ucheleweshaji.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Mifuko ya hifadhi (ISSA) Eliud Sanga amesema kuwa Shirikisho hilo litaendelea kuhimiza Mifuko hiyo kutimiza wajibu wake katika kutoa mafao bora kwa wanachama wao pamoja na kubuni mafao mapya ili kuwavutia wanachama.

Sanga amesema kuwa kwa sasa mifuko hiyo imefungua milango yake wazi kuwapokea wanachama kutoka sekta ambazo si rasmi ili nao waweze kunufaika na mafao .

IMG_2961