Mashindano ya Mapinduzi yanayofanyika kila mwaka visiwani Zanzibar yanatarajia kuanza kufanyika Januari 2 kwa kushirikisha timu kutoka Tanzania Bara, Kenya na Uganda.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka visiwani Zanzibar Kassim Haji Salum amesema Klabu za Gor Mahia ya kenya , KCCA ya Uganda , Yanga, Simba, Azam FC na Mtibwa sugar kutoka Tanzania Bara na Mafunzo na JKU kutoka visiwani Zanzibar ndio Timu zitakazoshiriki katika michuano hiyo
Katibu huyo aliongeza kuwa Michuano ya Mapinduzi Cup itazisaidia Timu za Yanga, Azam FC, JKU na Mafunzo kujiandaa na Mashindano ya CAF ya Klabu Barani Afrika .
Yanga watacheza michuano ya ligi ya mabingwa Afrika kwa kucheza mchezo wa mtoano na Timu ya Cercle de Joachim ya Mauritius wakati Azam FC watacheza na Mshindi kati ya Klabu ya Seychelles na Bidvest Wits ya Afrika Kusini katika Kombe la Shirikisho.
Mafunzo ya zanzibar wao watacheza na klabu ya AS Vita ya Congo DR kwenye CAF Champion Ligi na Timu ya JKU itashiriki Kombe la Shirikisho pamoja na Gaborone United ya Botswana.