Michuano Ligi Daraja la Kwanza na ratiba

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura

MICHUANO ya Ligi Daraja la Kwanza hatua ya makundi msimu huu inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini inaanza Oktoba 15 mwaka huu. Jumla ya timu 18 zinashiriki katika ligi hiyo.

Kundi A kesho itakuwa Temeke United vs Polisi Dar es Salaam (Uwanja wa Mlandizi, Pwani) na Mgambo Shooting vs Transit Camp (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga). Mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Burkina na Morani itachezwa Oktoba 16 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mechi za kundi B kesho ni Polisi Iringa vs Small Kids (Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora, Iringa), Tanzania Prisons vs Mbeya City (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya) na Mlale JKT vs Majimaji (Uwanja wa Majimaji, Songea).

Kundi C kesho ni AFC vs Manyoni (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Polisi Morogoro vs 94 KJ (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Polisi Tabora vs Rhino (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).

Ligi hiyo itaendelea tena Oktoba 19 mwaka huu kwenye viwanja tofauti. Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 30 mwaka huu na kupisha dirisha dogo la usajili litakaloanza Novemba 1 hadi 30 mwaka huu. Mzunguko wa pili wa ligi hiyo utaanza Januari mwakani.

LIGI KUU YA VODACOM
Mechi za wiki hii za Ligi Kuu ya Vodacom ni kama ifuatavyo;
Oktoba 15- JKT Ruvu vs Azam (Uwanja wa Chamazi)
Oktoba 16- Simba vs African Lyon (Uwanja wa Taifa)
Oktoba 19- Simba vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Chamazi)
Oktoba 20- Yanga vs Toto Africans (Uwanja wa Taifa)
Oktoba 21- Azam vs Polisi Dodoma (Uwanja wa Chamazi)
Oktoba 22- Simba vs JKT Ruvu (Uwanja wa Taifa)
Oktoba 23- Yanga vs Oljoro (Uwanja wa Chamazi)

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)