Michael Yombayomba Kupambana na Said Omar Kuchangia wagonjwa wa Moyo

Saidi Omari ‘Gogo Poa’ .kushoto na Rajabu Mhamila’Super D’

MABONDIA wazamani walioiletea nchi Medali katika mashindano ya All Africa Games na Jumuiya ya Madola miaka ya 1998, Michael Yombayomba na Said Omari ‘Gogo Poa’ wamejitolea kupanda ulingoni na kutwangana kwa ajili ya kuchangia watoto wenye matatizo ya Moyo.
Yombayomba ambaye alitwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya Jumuia ya Madola katika miaka hiyo ya 1998 na Gogo Poa wameamua kutwangana ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa watoto hao huku wakisisitiza wadau kuunga mkono tukio hilo.
Akizungumza na gaazeti hili Gogo Poa alisema pambano hilo litafanyika Januari 25 mwakani ambapo pia litasindikizwa na mapambano ya mabondia mbalimbali wenye viwango vya juu nchini.
“Tumeguswa sana na tatizo hili la watoto wanaougua ugonjwa wa moyo ambao wengi wao hukosa fedha kwa ajili ya matibabu hivyo sisi kama sehemu ya jamii tutahamasisha uchagiaji wa fedha kwa kujitolea kupanda ulingoni na chochote kitakachopatikana itakuwa ni sehemu ya mchango wetu,”alisema Gogo Poa.
Aliwaomba wadhamini na wadau mbalimbali kujitokeza kuzamini mchezo huo ambao una tija ya kuchangia watoto hawo kwani ata wao walikuwa watoto ndio mana wamekuwa katika afya nzuri na kucheza mchezo huo na kuiletea sifa taifa hili kwa kuleta Medali
Hivyo na watoto hawo wanatakiwa wawe na AFya njema ili wapate kuja kurithi nyayo zetu bila afya ya mtoto michezo yote akuna kwa kuwa vipaji vingi vinangaliwa ukiwa mtoto