Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Fundi Sanifu Bi Jemina Sadatale kutoka Mradi wa Umeme Jua wa KKKT Mpwapwa unaofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza kwa makini mtaalamu Bw. Godwin Msigwa kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Ensol Tanzania Limited inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini REA) alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) Bw. Bruno Mteta juu ya shughuli zinazofanywa na wakala huo mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo juu ya matumizi ya gesi kwenye magari kutoka kwa mtaalamu Bw. Charles Sangweni kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) mara alipotembelea banda hilo. Anayesikiliza ni Bw. Aloyce Tesha ambaye ni msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini.
Meneja Uhusiano kutoka Wakala wa Umeme Vijijini Bi. Jaina Msuya akimpokea Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa heshima wakati akiingia kwenye banda la Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ili kujionea shughuli zinazofanywa na wakala huo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya bunge Dodoma
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa mkufunzi wa Chuo cha Madini Dodoma Bw. Dickson Kaijage juu ya kozi zinazotolewa na chuo hicho mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma