MH. KOMBA AMETUMWA BUNGENI AKALALE?

Kwa mpango huu ndugu zangu tutafika? Baadhi ya waheshimiwa wetu wamekuwa ni watu wa kuhudhuria vikao tu, na mara nyingi huwa wanalala wakati vikao vya kujadili maslahi ya nchi vikiendelea. Hilo pozi la Mh. John Komba, ambaye ni mbunge wa Mbinga Magharibi linaonyesha kabisa kwamba amejiweka “comfortable” ili aweze kupata kauisingizi kidogo. Nafikiri utakubaliana na mimi kwamba mapozi mengine huwa yanaonyesha kwamba mtu alikuwa anajitahidi asilale…..lakini sio hili la Komba! Nchi yetu ipo katika hali mbaya sana kiuchumi, kijamii na kisayansi, hivyo basi ni muhimu kwa kila mTanzania (haswa wabunge) kuwa macho na kufahamu kinachoendelea ili waweze kutoa michango sahihi kwa maendeleo ya taifa letu.

Picha kwa hisani ya Mtandao.