Na Janeth Mushi, Arusha
HATIMAYE mgomo wa daladala uliodumu kwa siku mbili mfululizo
katika jiji la Arusha umeisha jana na huduma hiyo ya usafiri
kuanza kutolewa kama kawaida,ambapo awali jeshi la polisi mkoani
hapa lililazimika kutumia mabomu ya machozi kwatawanya wapiga
debe na madereva waliokuwa wakifanya fujo zilizosababisha
uharibifu wa mali yakiwemo magari ya serikali na ya watu binafsi.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana Mwenyekiti wa Baraza
(SUMATRA) la watoa ushauri na kutetea watumiaji wa usafiri wa
vyombo vya nchi kavu na majini Amani Lukumay, alisema kuwa mgomo
huo umemalizika kwa mashari yaliyotolewa na madereva hao ambayo
yanatakiwa kutimizwa ndani ya wiki moja huku mengine yakitakiwa
kutimizwa ndani ya siku mbili .
Mwenyekiti huyo alisema kuwa masharti hayo ni pamoja na kuwekwa
kwa alama za barabarani katika maeneo yote ya mjini hapa,alama
zitakazoonyesha mahalai panaporuhusiwa kupakia na kushushia abiri
na yale ambayo hatyataruhusiwa.
Aliongeza kuwa sharti lingine ni kwa wale wafanyabiashara wadogo
wadogo maarufu kama “Machinga” wanaofanya biashara zao katika eneo
la stendi kuondoka mara moja kutokana na wafanyabiashara hao
kutandaza biashara zao chini ambapo watu wanatakiwa kupita.
“Madai mengine ya madereva hao ni pamoja na magari ya watu binafsi
ambao wengi wao ni wale wenye maduka katika kituo hicho kidogo cha
mabasi kuwa yaondolewe kuanzia jana ili madereva hao wa daladala
waweze kupata mahali ya kupaki magari yao na kuepusha usumbufu
unaojitokeza wakati wa abiria kupanda na kushuka toka ndani ya
daladala hizo”alisema Lukumay
Lukumaya alisema kuwa mbali na madai hayo mengine ni pamoja na
kuongezwa kwa muda wa kufungwa kamba katika kituo hicho ambapo
kamba hufungwa kuanzia saa 12jioni hali inayosababsiah usumbufu na
badala yake iwe inafungwa saa 4 usiku.
.
“Madai mengine ya madereva hao ni yele ya kutaka wenzao ambao
wanashikiliwa na jeshi la polisi kuachiwa huru,ambapo AKIBOA
wanashughulikia suala hilo ili kuweza kuwawekea dhamana watu hao
wanaoshikiliwa”alisisitiza Mwenyekiti huyo
Aidha pamoja na daladala hizo kusitisha mgomo waliokuwa wameuweka
kwa takribani siku mbili,Lukumaya alisema leo wanatarajia kukutana
katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha Raymond Mushi pamoja na
uongozi wa Manispaa ya jiji la Arusha, madereva,wamiliki wa
magari,makondakta,SUMATRA,AKIBOA,TANROADS pamoja na polisi wa
usalama barabarani ili kuweza kujadili utekelezaji wa makubaliano
hayo yaliyoafikiwa pamoja na namna ya kutatua changamoto
zinazoikabili sekta hiyo ya usafirishaji.
Lukumay aliwataka wakazi Jijini hapa kutoa taarifa za wanaokiuka
amri ya SUMATRA na kupandisha nauli kinyume na sheria,ili waweze
kuchukuliwa hatua kali za kisheria na kuwataka madereva kuzingatia
sheria zilizowekwa ikiwa ni pamoja na kutokupandisha nauli.
Hata hivyo pamoja na mgomo huo kusitishwa baadhi ya magari
hayajarudi barabarani na yaliopo ni machache ikilinganishwa na
yanavyokuwa siku za kawaida huku katika eneo Unga Ltd kukiwa
hakuna hata daladala moja inayotoa huduma ya usafiri kwa madai
kuwa , madereva wenzao na makondakta 60 wako ndani, jambo
linalopingwan na mwenyekiti huyo na kubainisha kuwa ambaow
anashikiliwa ni watano(5).